fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Facebook Intaneti Teknolojia

Live Audio Rooms – Facebook kuja na ClubHouse yao, na mengine mengi hivi karibuni

Live Audio Rooms – Facebook kuja na ClubHouse yao, na mengine mengi hivi karibuni

Facebook wanakuja na Live Audio Rooms, huduma kupitia Facebook inayoruhusu mtu mmoja kuandaa chumba cha maongezi kwa njia ya sauti (audio) na kurusu wageni wasikilizaji au wachangiaji mada.

app ya clubhouseHuduma kama hiyo imefanywa kuwa maarufu kutokana na app ya ClubHouse, app inayokua kwa kasi kwa watumiaji wa iPhone. Watu wengi walikuwa na mtazamo ya kwamba kuchelewa kwa app hiyo kuwafikia watumiaji wa Android kunaweza kuwapa nafasi wengine kama Facebook au Twitter kuingia na kufanikiwa kwenye huduma kama hiyo.

Katika taarifa yao Facebook wamesema wanafanyia kazi vitu vipya kadhaa ambavyo vinahusisha teknolojia ya sauti.

  • Audio Rooms – Uwezo kufanya vikao kwa njia ya sauti, kuhusisha watu wawili au zaidi.
  • Soundbites – Uwezo wa watu kurecord ujumbe wa mfupi wa sauti na kuweza kupost kama wanavyopost ujumbe wa picha, video na maneno kwa sasa.

Soundbites – Post za Sauti

  • Pia uwezo wa kusikiliza Podcast – vipindi vya kwa njia ya sauti. Fahamu zaidi kuhusu Podcast.
  • Live Audio Rooms – Huduma inayofanana na ile ya app ya Clubhouse, uwezo wa mtu kuanzisha mazungumzo/mijadala na kuruhusu watu wengine kuwa washiriki wa mijadala na wengine kuwa wasikilizaji tuu.
live audio rooms

Facebook watawezesha vyumba hivi vya mazungumzo kuwa na uwezo wa kuchangia kwa vitendo masuala ya misaada n.k.

Facebook hawajatoa rasmi tarehe husika ya sisi kuweza kuona hivi vikija ila wamesema vyote vipi katika hatua za maboresho na tuweze kuzitegemea kuanza kupatikana katika kipindi cha miezi michache ijayo.

Facebook wamekuwa maarufu sana kwa kuiba mawazo mapya ya apps zingine ndogo – kama vile walivyofanya kwenye teknolojia ya Status kutoka Snapchat, au Reels – video za Instagram za ambapo ni kitu wamechukua kutoka TikTok.

App ya Clubhouse imekuwa maarufu kwa watumiaji wa iPhone na inaonekana kuchelewa kwake kuwafikia watumiaji wa Android kuna weza changia kwa kiasi kikubwa mafanikio kwa Facebook ambao inategemewa watawahi kuleta Live Audio Rooms kabla ya Clubhouse kufika kwa watumiaji wa Android.

Chanzo: Facebook

SOMA PIA  NASA Waja na teknolojia mpya ya WiFi - Kutumia Chaji Kiasi Kidogo Zaidi
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania