fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Teknolojia

Uwezo wa programu tumishi kujifuta kupelekwa kwenye Android za zamani

Uwezo wa programu tumishi kujifuta kupelekwa kwenye Android za zamani

Spread the love

Ingawa baadhi ya simu kuondolewa kwenye mpango wa kupokea masasisho mbalimbali kutokana na kwamba kuonekana kuwa muda wake umeshafika wa kuwekwa kando lakini mara moja moja huwa zinakumbukwa Android za zamani.

Hivi sasa toleo la Android limefikia namba 11 huku Android 12 ikiwa haiko mbali kutoka lakini hadi leo kuna watu simu zao zinatumia programu tumishi toleo ambalo Google imeshaziweka kando kuwweza kuhama kutoka toleo moja hadi nyingine halikadhalika kupokea masasisho.

SOMA PIA  Sababu Kwanini Hutakiwi Ku 'Hibernate' Laptop Yako!

Hata hivyo, rununu hizo ambazo zinatumia toleo mbalimbali la nyuma mathalani Android 6, 7 na wengineo wamekuwa wakikumbukwa kwa kupelekewa maboresho kama ambavyo kwenye Android 11 inawezekana kupanga kuondoa programu tumishi ambazo mtu hazitumii mara kwa mara baada ya muda fulani kupita sasa kuletwa na huku chini.

Ndio, Google inapanga simu janja ambazo zinatumia Android 6 kwenda juu kwa programu tumishi kujiondoa zenyewe tuu iwapo hazitatumika ndani ya kipindi fulani. Hii inawezekana kuweka pale ambapo mtu anapakua programu tumishi anaweza akaruhusu mathalani TikTok kujifuta yenyewe tuu iwapo haijatumika kabisa ndani ya kipindi fulani.

Android za zamani

Programu tumishi ambazo zilitengenezwa kutumika kwenye Android za zamani inabidi mtu mwenyewe aende kukiruhusu kipengele kinachowezesha kitu husika kujifuta iwapo haijatumika kwa miezi kadhaa.

Kipengele hiki kitasaidia vilivyo kufanya simu janja kutojaa nafasi bila ya sababu za msingi kwani kuna watumiaji ni wavivu kupunugza programu tumishi ambazo hawazitumii mara kwa mara; kwa lugha rahisi tunajua kuzipakua tu na si kuziondoa. Je, wewe una mawazo gani kuhusu habari hii?

Vyanzo: Engadget, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania