WhatsApp Messenger App sasa ina watumiaji wengi walio ‘active’ kuliko Twitter haya yamethibitishwa na afisa mtendaji mkuu wa WhatsApp Jan Koum. Amesema pia sio tuu kuipita Twitter ambayo ina watumiaji milioni 200 waliko active kwa mwezi Bali pia inahusika hadi na kutuma meseji zaidi ya bilioni 20 kwa siku.
WhatsApp imepata jina kubwa kwakua ni njia rahisi ya kutuma na kupokea meseji nje na ndani ya nchi bila kutumia makato ya mitandao ya simu zaidi ya internet.
Watu wanajiuliza kampuni ya WhatsApp inapata vipi faida yake wakati haijaruhusu matangazo katika Application yake? Jan Koum alisema “Tuna njia mbadala ya kupinga matangazo na tunajisifu kwa hilo. Nani angependa kuona matangazo wakati akiwa anawatumia meseji wapendwa wake?.Tumezungukwa sana na matangazo katika maisha yetu ya kila siku na Simu sio sehemu ya matangazo, Simu zetu zimeungana nasi kiundani na kuweka matangazo kwenye simu si jambo jema”
Badala ya hivyo WhatsApp imeamua kijikita zaidi katika njia ya kipekee ambayo inahusisha watumiaji wa WhatssApp kuilipia Application hiyo kwa mwaka kwa kiasi cha Dola 1.
No Comment! Be the first one.