CEO wa kampuni ya simu za Blackbery, Thorsten Heins anategemea watumiaji wote wa vyombo vya mawasiliano haswa simu na kompyuta kutokua na haja ya kutumia Tableti ndani ya miaka mitano ijayo.
Bwana Heins amesema “Ndani ya miaka mitano sitegemei kama kutakua na sababu ya kutumia Tableti tena” na akaongezea kwa kusema “labda skrini kubwa katika mahali unapofanyia kazi lakini sio Tableti kama hivyo.Tableti zenyewe hazipo katika mfumo mzuri wa kufanyia kazi”
Amesema ndani ya miaka hiyo anaiona blackberry kufanya vizuri sana katika mfumo wa simu na computer na hilo ndio tegemeo lao. Pia akasema anataka kupata asilimia kubwa ya soko kadri anavyoweza ila sio kwa njia ya kukopi. Bwana Heins anajiamini kwa kuwa kaipatia kampuni hiyo ya Blackberry iliyokuwa inajulikana kama RIM (Research In Motion) matunda makubwa tangia alivyojiunga na kampuni hiyo mwaka 2007.
Je utabiri wa bwana Heins utatimia kama anavyofikiria? tungojee tuone…
No Comment! Be the first one.