fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Teknolojia

Fahamu Android M: Toleo jipya la Android Baada ya Lollipop

Fahamu Android M: Toleo jipya la Android Baada ya Lollipop

Spread the love

Katika mkutano mkubwa katika jiji la Francisco huko nchini Marekani masaa machache yaliyopita kampuni ya Google imetambulisha mambo mbalimbali, kuna mapya na yale yanayoboreshwa zaidi. (Kusoma bofya hapa – Fahamu Mambo Yote Makubwa Yaliyotangazwa na Google). Katika habari zilizokuwa zikisubiriwa zaidi ni pamoja na zile zinazohusu toleo lijalo la programu endeshaji ya Android baada ya hili la tano linalofahamika kama Android Lollipop.

Toleo lijalo la Android kwa sasa linafahamika kama Android M, jina rasmi litatangwaza baadae zaidi na toleo hili litapatikana miezi kadhaa baadae mwaka huu ila kwa sasa fahamu nini kipya kinakuja.

Muonekano;

android-m-google

Kimuonekano bado kwa asilimia kubwa inafanana kwa kiasi kikubwa na toleo la sasa la Android Lollipop, hasa kupitia ubunifu wa kimuonekano unaofahamika kwa jina la Material Design (Kusoma kuhusu Ubunifu huu bofya hapa )

Mabadiliko katika jinsi Apps zinapakuliwa (Kuwa ‘installed’)

Kwa sasa kama utakuwa unakumbuka vizuri apps ukiwa unapakua kwenye simu yako zitakuonesha kwa ufupisho tuu ya kubwa zitakuwa zinatumia nini kwenye simu yako. Kwa mfano app kama WhatsApp itakwambia itaitaji kusoma namba zako (phonebook) ziku zote, pia itataka uwezo wa kutumia kamera n.k. Katika matoleo ya nyuma ulikuwa unasoma na uwezi kuchagua ni kitu gani ukatae katika urodha ya vitu vyote vinavyoitajika ili app hiyo kufanya kazi. Hili limekuwa likilalamikiwa na wengi na sasa Google wameleta mabadiliko.

Muonekano wa eneo (dashboard) utakaloweza kuwa unaenda na kufanya mabadiliko ya ruhusu za app husika
Muonekano wa eneo (dashboard) utakaloweza kuwa unaenda na kufanya mabadiliko ya ruhusu za app husika
SOMA PIA  Samsung Waja na Galaxy Tab S2, Tableti Nyembaba Zaidi Duniani

Kuanzia sasa ata pale utakapokuwa unafanya masasisho (updates) utaweza kukubali na kukataa baadhi ya ruhusu (permissions) kwa app husika. Hii itasaidia katika kulinda data za mtumiaji dhidi ya apps zinazokuwa zinatumia vitu visivyokuwa na ulazima au bila ya wewe kufahamu.

Utaweza kukataa au kukubali kuipa ruhusu app kutumia au kufanya kitu katika simu yako

Utaweza kukataa au kukubali kuipa ruhusu app kutumia au kufanya kitu katika simu yako

Utaweza kwenda kwenye eneo katika Android M na kuweza kuchagua na kukataa ruhusu mbalimbali za apps unazotumia kwenye simu yako.

Uhusiano wa kiutendaji kazi kati ya Apps na Kivinjari cha Chrome yaboreshwa

Google wanataka kukupunguzia hatua za kubofya hadi uweze kufungua kitu kutoka kwenye app kwenye kivinjari, mfano pale unapotakiwa kufungua linki (mtandao). Kuanzia sasa kwa apps zilizotengenezwa na kupewa uwezo wa kutumia kivinjari cha Chrome moja moja basi linki zako zitaweza kufunguka kwa urahisi bila kukuhamisha kutoka kwenye app unayotumia kwenda kwenye Chrome. Jiandae kusahau lile chaguo la ‘Open With’..

Utumiaji wa chaji mdogo zaidi pale simu ikiwa haitumiki

Suala la chaji ni jambo linalowaumiza kichwa wengi sana na Google pia huwa wanajitaidi kuja na vitu vipya katika matoleo yake ya Android kukabiliana na suala la chaji. Katika toleo hili la Android programu endeshaji hiyo imepewa uwezo wa kuingia kwenye kitu walichokiita ‘usingizi mzito’, yaani kama vile ‘hibernation’ katika kompyuta. Kupitia teknolojia ya kutambua kama inatumika au imeachwa tuu basi simu itaweza kujiingiza kwenye usingizi mzito pale ambapo itakuwa haitumiki.

Tofauti ya mambo yanayofanya kazi pale unapokuwa unaitumia simu na pale ambapo utakuwa hauitumii
Tofauti ya mambo yanayofanya kazi pale unapokuwa unaitumia simu na pale ambapo utakuwa hauitumii
SOMA PIA  Tofauti Kati Ya 'Personal', 'Business', Na 'Creator' Akaunti Huko Instagram!

Ikiwa katika usingizi mzito simu itazima apps zote zisizokuwa za msingi ila itaendelea kuwa na uwezo wa kupokea sms, simu na habari mpya (notifications) muhimu ila katika hapa itakuwa inawasiliana na huduma hizi zingine zisizo za msingi kwa kiwango kidogo sana na hivyo kutumia chaji kwa kiasi kidogo sana. Google wamesema walifanya majaribio kati ya simu isiyokuwa na teknolojia hiyo yaani ya Android Lollipop dhidi ya simu yenye teknolojia hiyo yaani Android M na wakakuta simu ya Android M inaweza kukaa na chaji mara mbili zaidi pale zilipoachwa kutumika (Walitumia Nexus 6 katika majaribio hayo).

Google Now yaboreshwa

Hii ni app moja nzuri sana kama wewe unatumia huduma za Google sana, yaani GMail, Google Maps, Google Search na nyinginezo. App hii kwa sasa itakuja na uwezo mkubwa zaidi, kwa mfano pale unaposikiliza mziki unaweza uliza jina la msanii wa nyimbo hiyo na ikakutajia. Pia itaweza kujibu maswali ya muvi n.k. Pia app hii katika Android M itaweza kupatikana kwa urahisi kwa kubofya mara mbili sehemu ya ‘Home’ kwenye simu yako.

SOMA PIA  Messenger Rooms kwenye WhatsApp

Uwezo wa teknolojia ya malipo ya Android Pay

Wakati katika nchi zetu huduma za malipo ya simu kupitia mitandao ya simu imeshikilia kwa kasi katika nchi kama Marekani njia hizi za malipo ndio zinaanza kuonekana muhimu sana
Wakati katika nchi zetu huduma za malipo ya simu kupitia mitandao ya simu imeshikilia kwa kasi katika nchi kama Marekani njia hizi za malipo ndio zinaanza kuonekana muhimu sana

Toleo hili linakuja na teknolojia ya malipo kwa kutumia simu inayofahamika kwa jina la Android Pay, ni huduma mpya kutoka Google (Isome zaidi hapa – )

Huduma mpya ya Google Photos

Huduma za kuhifadhi, kuboresha na kufanya mabadiliko ya kimuonekano wa picha za ukubwa mbalimbali imeanzishwa na kupewa jina la Google Photos. Ingawa huduma hii itaanza kupatikana mara moja kwenye soko la apps la Google Play na Apple Store app hii itakuja moja kwa moja katika toleo la Android M. Soma zaidi kuhusu huduma hii – Fahamu Mambo Yote Makubwa Yaliyotangazwa na Google

Hayo ndiyo makubwa kuhusu toleo lijalo la Android. Je ni habari gani imekufurahisha zaidi kuhusu toleo hili la Android? Je unaweza kuotea katika Android M, M inasimama kwa ajili ya nini? – Kumbuka Google huwa wanatumia majina ya vyakula katika matoleo ya Android.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. hussein hemed - May 29, 2015 at 12:09 - Reply

    naombeni msaada nimenunnua sim toka ebay ni orginal sony tx imel;353596050071588; haina play store wa google account yani kitu chochote kile cha google hakikubali sielewi nimewasiliana na muuzaji ameniambia ni donwload market ila brouza yake haikubali nisaidieni:email husseinhemed30@yahoo.com
    0759337836

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania