Mwezi Septemba una simu janja kadha kadha ambazo tayari zimeshazinduliwa na bado kuna nyingine zipo njiani kuja hivyo kuna vingi ambavyo bado hatujaviona kutoka makampuni mbalimbali. Redmi 10 Prime ni ingizo jipya ndani ya familia ya Redmi.
Ukizungumzia simu janja mpya kutoka kwenye familia ya Redmi basi Redmi 10 Prime ndio toleo jipya ambalo limetengenezwa kwa ajili ya kutumika kufanya vitu vingi kwenye simu janja. Kuanzia mwonekano, memori, kamera vyote vimejitosheleza. Sifa zake ni kama ifuatavyo:-
Kioo :
- Ukubwa: inchi 6.65
- Ubora: LCD (1080*2400px, 90Hz); ung’avu wa hali ya juu sana+ kamera ya mbele ipo katikati (inagawa kioo cha mbele nusu kwa nusu)
Memori :
- Diski uhifadhi: 64GB/128GB+sehemu ya kuweka memori ya ziada
- RAM: GB 4/6
Kamera :
- Kamera Kuu: MP 50, 8 na mbili zina MP 2+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
- Kamera ya Mbele: MP 8+Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
Betri/Chaji :
- Li-Ion 6000 mAh
- USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 18W, 9W za kuchaji simu nyingine kwa kutumia waya
Kipuri mama :
- MediaTek Helio G88
Uzito :
- Gramu 192
Programu Endeshi
- MIUI 12.5, Android 11
Rangi/Bei :
- Nyeupe, Nyeusi na Bluu
- GB 4/64-$170.99 (zaidi ya Tsh. 393,277) na GB 6/128-$198.35 (zaidi ya Tsh. 456,205) bei ya India
Septemba 7 ndio siku ambayo simu hii inaingia sokoni huko India. Je, unaizungumziaje bidhaa hii? Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.