Eesha Khare ni msichana Wa kihindi mwenye urai wa marekani ambae ameweza kutengeneza kifaa kinachochaji simu kwa sekunde 20. Eesha ana umri wa miaka 18 na ni mwanafunzi katika shule ya ‘Lynbrook High school’ iliyopo California. licha ya kuwa na umri mdogo pia ameweza kuwa mshindi wa ‘Intel Awards” mwaka 2013. kifaa hicho kinaweza chaji simu kwa sekunde 20 pia kinahifadhi chaji mda mrefu kuliko kifaa kingine.Utengenezaji wa kifaa hicho umemsababishia ashinde dola 50,000 kama zawadi katika ‘the Intel Foundation Young Scientist Award’ iliyofanyika Phoenix, Arizona.kifaa hicho ni kidogo sana kwa umbo kinakaa na chaji kwa mda mrefu na kinawasilisha chaji kwenye betri kwa mda mchache sana. Baada ya kutengeneza kifaa hicho hapo aliteka hisia za Google Na makampuni mengine makubwa yanayojihusisha na teknolojia.
Fikiria ukiwa umetoka uko mjini siku nzima na simu yako haina chaji, hata kama ukiwa umebeba chaja bado itabidi utafute sehemu ya kuchajia mfano kwenye ‘Canteen’ yoyote hata hivyo bado utapoteza mda wako kuisubiria simu iingine chaji lakini kifaa hiki kinaweza tatua hayo yote kwa mda mchache sana
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Mbunifu na mpenda teknolojia.
Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM
Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.
| mhariri(at)teknokona.co.tz |
No Comment! Be the first one.