Nchini Tanzania hivi sasa wananchi wanakatwa tozo kwenye miamala ya simu ambapo serikali inachukua sehemu ya ada na nyingine inachukua kampuni inayotoa huduma za mawasiliano.
Julai 15 mwaka huu ndio tozo za kwenye miamala ya simu ambazo zinajumuisha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia kupata pesa kutokana na kutuma/kupokea simu kwa njia ya simu. Hata hivyo, yakatokea malamiko ambayo yalifanya wizara husika kufanya marekebisho ambapo serikali ilipunguza 30% na tozo mpya kuanza kutumika Septemba Mosi ya mwaka huu.
Watu wengi tuu wanafanya miamala kwa njia ya simu kila siku na kuingiza mamilioni ya pesa kwa makampuni ya simu halikadhalika serikali lakini si wengi ambao tunafahamu ni kiasi gani ambacho kinakwenda upande wa serikali. Sasa baada ya marekebisho hiki ndio ambacho serikali inachukua kulingana na muamala ambao mtu anaufanya.
Katika ulimwengu wa teknolojia na urahisi wa kutuma ama kupokea pesa kwa njia ya simu ni wazi kuwa wananchi wengi wanaendelea kufanya miamala na hata kuzoea tozo na makato mapya ambazo zimeanza kutumika tangu Septemba 1 ya mwaka huu.
No Comment! Be the first one.