Mwanamume mmoja nchini Uswisi apigwa faini kisa kubonyeza kitufe cha Like katika mtandao wa Facebook.
Mwanaume huyo ameingia matatani baada ya kubonyeza kitufe cha alama ya kupenda ama ‘Like’ katika maoni ya mmoja ya watumizi wa mtandao wa Facebook yaliyomshutumu mmoja ya wanaharakati wa kutetea haki za wanyama kuwa ni mbaguzi.
Mahakama moja ya ngazi ya wilaya mjini Zurich nchini humo ilimfungulia mtu huyo wa miaka 45 mashtaka kwa madai kuwa ali ‘Like’ maoni ambayo ni ya uchochezi na ya kuharibu hadhi ya mtu kupitia mtandao wa kijamii.
Kesi hiyo ilihusiana na maoni ambayo yalitolewa kumhusu mkuu wa shirika la kutetea haki za wanyama bwana Erwin Kessler.
Mwanaume huyo amepigwa faini ya Dola 4,100 ambzo ni takribani kwa pesa ya kitanzania ni Shilingi milioni Tisa. Mwanaume huyo amepewa nafasi ya kukata rufaa kama atataka kufanya hivyo.

Maoni hayo ya Facebook yaliandikwa mwaka 2015 ambapo mjadala ulikuwa ni wa kuchagua wanyama ambao wangetumika katika hafla ya maonyesho ya wanyama .
One Comment
Comments are closed.