fbpx

Ushindani katika vioo vinavyojikunja

0

Sambaza

Kadri siku zinavyokwenda na watu/makampuni mbalimbali yanazidi kuleta teknolojia zinazovutia, zenye ubunifu wa aina yake. Utakuwa umeshawahi kusoma makala zetu kuhusu vioo vinavyojikunja lakini kuna mshindani mwingine katokea.

Teknolojia/ubunifu ni moja ya vitu ambavyo havina mipaka na hivyo basi kampuni moja yenye makao yake jijini California, Marekani imeonekana kuwa kivutio kwa wengi kutokana na kile ambacho imetengeneza.

Royole imetengeneza kioo cha kutumika kwenye simu rununu ambacho kinaweza kujikunja na kuvaliwa  kwenye mkono kama bangili.

vioo vinavyojikunja

Simu rununu yenye kioo cha kujikunja, kioo chake ni aina ya OLED na wembamba wake ni 0.01mm.

Kampuni hiyo imeshafanya kazi na makampuni mbalimbali kutengeneza vioo vyenye teknolojia ya kujikunja kuanzia kwenye magari, spika, n.k. Washindani wengine ambao wanaonekana kuweka teknolojia hiyo ni Samsung, LG, Lenovo.

vioo vinavyojikunja

Teknolojia ya vioo vinavyojikunja inavyozidi kushika kasi.

Bidhaa hiyo bado haijatoka lakini wahusika wameahidi kuwa bidhaa zao zitakuwepo kwenye mkutano wa IFA utakaofanyika Berlin-Ujerumani kwa mwaka 2018.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Nokia kuingiza dola 3.48 kwa kila simu yenye 5G
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.