Suala la tozo kwenye miamala ya simu imekuwa ni mwiba kwa Watanzania kiasi kuibuka malalamiko mengi ambayo yamesababisha biashara kuyumba vilivyo lakini sasa serikali imesikia na kupunguza tozo.
Julai, 15 2021 itakumbukwa na wananchi wengi wa Tanzania kwani ndio tarehe ambayo tozo kwenye miamala ya simu ilianza kutumika lakini tangu kuanza kwa mabadiliko hayo ambayo yanahusisha moja kwa moja serikali, wananchi na makampuni ya mitandao ya simu mambo yamekuwa si shwari kwani kiwango cha mapato yanayotokana na miamala ya simu yameshuka mara dufu.
Kwa zaidi ya mwezi mawakala wa mitandao ya simu halikadhalika makampuni yanayosiamia biashara hiyo yamekumbana na wakati mgumu kwani wananchi hawafanyi miamala kwa wingi kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya tozo mpya kuanza kutumika.
Tofauti ndogo ya miamala ya simu yabainika
Kwa mujimu wa takwimu imeomekana kuna tofauti ndogo ya miamala ya simu ukilinganisha kabla na baada baada ya tozo hizo mpya kuanza kutumika. Kwa mujimu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa wastani miamala milioni 9.9 ilifanyika ndani ya siku moja na iliyofanyika ndani ya siku 28 ni zaidi ya 277.2 milioni; kabla ya tozo hizo mpya miamala 10-11 milioni ilifanyika kwa siku.
Mabadiliko yaliyofanyika
Zaidi ya mwezi mmoja tangu “Kodi ya kizalendo” kuanza kutumika serikali imeamua kupunguza tozo kwa asilimia 30 halikadhalika ada ya kutuma pesa kutoka mtandao mmoja wa simu hadi mwingine nayo imepunguzwa kwa 10% kufuatia mazungumzo baina ya serikali na makampuni ya mitandao ya simu nchini Tanzania.
Makato/tozo zilizopunguzwa na serikali Septemba Mosi 2021. Lengo la tozo/makato haya ni kutumia fedha hizo zinazopatikana katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa maendeleo ya Tanzania.
Vyanzo: Gazeti la Mwananchi, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.