fbpx
Tanzania, Teknolojia

Uwekezaji katika sarafu ya za kidijitali nchini Tanzania

uwekezaji-katika-sarafu-ya-za-kidijitali-nchini-tanzania
Sambaza

Miezi kadhaa iliyopita tulishawahi kuandaaa makala kuhusu orodha ya nchi ambazo zinajishughulisha na uwekezaji/kufanya miamala kwa njia ya pesa zisizoshikika au kwa lugha rahisi sarafu za kidijitali, Tanzania nayo ipo kwenye orodha hiyo.

Kama moja ya teknolojia ambayo inakuwa kwa kasi nchi mbalimbali duniani zinatambua na kukubali mfumo wa malipo kwa kutumia sarafu hizo za kidijiti huku nyingine zikiwa kwenye mchakato wa kuzikubali. Kwa Tanzania pia watu kadha wa kadha wamewekeza huko kutokana na kuamini mfumo huo.

INAYOHUSIANA  Machache kuhusu Nokia 7.1

Jitihada zinazofanyika Tanzania kuleta mbele sarafu za kidijiti.

Kwa kuanza tuu ipo jumuiya (Blockchain Tanzania) ambayo inalenga kuelimisha umma/Watanzania kuhusu teknolojia iliyopo nyuma ya sarafu husika kwa maana ya kwamba mtu anaweza akawekeza na kupata faida baada ya muda fulani ila kabla ya kujiingiza huko basi ni vyema ukapata elimu na kuelewa kisha ufanye maamuzi ya kuwekeza.

Uwekezaji
Baadhi ya wanajumuiya wanaofanya kazi ya kuelimisha umma kuhusu sarafu za kidijitali pamoja na teknolojia yake.

Lakini bado yapo makampuni nchini Tanzania yanafanya biashara hiyo hata kuwa na sarafu zake zenyewe mathalani TemboCoin ambayo tayari inafanya kazi lakini pia iRA na sarafu yake ya Diligence ingawa bado haijaingia sokoni.

Kubwa zaidi hivi karibuni Belfrics Tanzania Limited walipata fursa ya kueleza mbele ya baadhi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kuhusu faida sarafu za kidijitali na wengine serikali ikaweza kutambua kama njia mojawapo rasmi inayoweza kutumia kufanya miamala.

Uwekezaji
Wabunge mbalimbali wakiangalia kile ambacho Belfrics Tanzania iwaletea mbele ya macho yao.

Kiujumla jitihada mbalimbali zinaendelea kuifanya Tanzania nayo iwe miongoni mwa nchi ambazo zinatambua rasmi mfumo wa malipo kwa sarafu za kidijitali au uwekezaji wa aina hiyo.

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Marufuku matumizi ya Bitcoin nchini Iran - TeknoKona Teknolojia Tanzania
    July 16, 2019 at 3:01 am

    […] Makamu wa rais-benki kuu, Nasır Hakimi amesema kuwa serikali ya Iran imepiga marufuku shughuli zote za matumizi ya sarafu ya kidijiti-Bitcoin. […]