fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

LG Watoa Keyboard Yao Ya 2 Ndogo Na Ya Kujikunja Ikiwa Na Mistari 5 Ya Vibonyezo!

LG Watoa Keyboard Yao Ya 2 Ndogo Na Ya Kujikunja Ikiwa Na Mistari 5 Ya Vibonyezo!

Spread the love

Kampuni la LG kutoka korea, limetengeneza keyboard ndogo ambayo inaweza kutumika kwenye vifaa kama vile kompyuta n.k. Keyboard hii ni ndogo sana kwa umbo na la kuvutia zaidi ni kwamba inakunjika


Keyboard hii imepewa jina la ‘Rolly Keyboard 2’ na kampuni inawahakikishia watumiaji kuwa na urahisi wakati wanaitumia katika kufanya kazi zao mbali mbali kama vile kuandika vitu.
Mara ya kwanza LG walitoa Keyboard ya chini yake ambayo waliipa jina la ‘LG Rolly’ na sasa wamekuja na toleo la pili la keyboard hiyo.

Muonekano Wa Keyboard Hiyo

Muonekano Wa Keyboard Hiyo

Cha kuvutia kingine katika keyboard hiyo ni kwamba ina mistari mitano tuu ya vibonyezo. Uchache wa mistari hiyo ya vibonyezo unaiwezesha Keyboard hii kujipatia umbo dogo kabisa.

Mambo mapya katika keyboard hii ni kibonyezo cha TAB ambacho kimewekwa kwa upande wa chini mwishoni mwa vibonyezo vingine. Pia LG wameboresha katika uwezo wa huduma ya Bluetooth katika kifaa hiki.

Keyboard Hiyo Ikiwa Imehifadhiwa Inachukua Umbo Dogo

Keyboard Hiyo Ikiwa Imehifadhiwa Inachukua Umbo Dogo

Kifaa hiki kinakuja na betri lile la mfumo wa 1 AAA. Kwa sasa keyboard hii ambayo inatumia mfumo wa QWERTY inapatikana kwa wateja ambao wapo korea. LG hawataishia hapa kwani keyboard hii ni ya aina yake kwa hiyo wana mipango mikubwa ya kuongeza soko lao kwa kuvuka mipaka.

SOMA PIA  Miwani kwa ajili ya watu wafupi kuweza kuona mbali

Kingine cha kuvutia zaidi kuhusiana na keyboard hizi ni kwamba zinaweza zikatumika katika simu za iOS, Android na Windows

Niambie je ikija kwa Tanzania utakuwa wa kwanza kuinunua? Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari kadha wa kadha za kiteknolojia.Kumbuka Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania