fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao wa Kijamii Teknolojia

Vine Waboresha Jinsi Ya Kuangalia Video!

Vine Waboresha Jinsi Ya Kuangalia Video!

Spread the love

Vine inametoa maboresho au masashisho mapya katika App yake. Maboresho hayo yatakuwezesha mtumiaji wa App hiyo kuweza kuangalia video mbali mbali katika chaneli zako kwa urahisi


Waboreshaji (developers) wa vine wametangaza Aprili 13 kuwa App hiyo ina maboresho kabambe katika swala zima la kuangalia Video. Boresho kubwa lililofanyika ni kwamba mtumiaji wa mtandao huo anaweza akacheza video zote katika cheneli Fulani anayoipenda kwa ku ‘click’ sehemu moja (Sehemu ya ‘Watch’)

Kabla ya hapo watumiaji wa App ya Vine iliwabidi kwanza wachague video moja moja ili kuzicheza. Yaani ulikuwa unachagua video moj, unaicheza na kisha ukimaliza unachagua video nyingine ili kuitazama

App Ya Vine

App Ya Vine

Vine inavyoonekana ni kwamba ndio kampuni moja tuu ambalo limewekeza katika video tuu. Kumbuka makampuni mengine kama vile Facebook na Mengine yanakuwa yana mambo tofauti tofauti ukiachana na video tuu.
Ukiangalia linaweza kuwa jambo zuri kwani kwa sasa Video zimekuwa na muamko mkubwa sana katika mitandao ya kijamii. Lakini kibaya kuhusu kuwekeza ni kwamba kuwekeza pesa nyingi katika eneo moja au katika bidhaa moja inaweza ikawa ni mbaya. Hapo unaweza ukapata hasara kubwa kama mambo yakienda kombo.

SOMA PIA  Kongamano Kubwa la Masuala ya Teknolojia Kufanyika Jijini

Lakini pia ukiangalia katika upande mwingine ni kwamba unaweza ukapata faida kubwa tuu kwani teknolojia kila siku inakuwa na kwa sasa video ndio zimeshika chati katika mitandao ya kijamii.

Video za Vine zina urefu wa sekunde 6 tuu lakini zina sifa kubwa za kuwaburudisha watu. Pata picha kama una chaneli yako ambayo inaweka video za kuchekesha kwa kuchagua sehemu ya ‘Watch” katika chaneli hiyo unaweza ukaangalia video zote kwa mkupuo huku ukiwa unavunjika mbavu

Muonekano Wa Eneo La Watch Katika iPhone 6

Muonekano Wa Eneo La Watch Katika iPhone 6

App ya Vine katika iOS pia na Android ina njia ya kuzipangilia video zake. Kwa mfano kupangilia kulingana na video zinazofanana au hata video maarufu zaidi. Kupangia huku kunawawezesha watumiaji kupata urahisi katika kuweza kuangalia video hizo.

SOMA PIA  Fahamu jinsi ya kutengeneza Xpress Account kwenye App ya Ecobank

Watumiaji wa iOS na Android wanaweza wakapata huduma hii mpya ya Vine kwa kusasisha matoleo ya App hiyo.

Niambie hii boresho umelipokeaje? Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Usisahau kutembelea Teknokona kila sikua kwa habari na maujanja ya teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania