fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
instagram Mtandao wa Kijamii Snapchat Teknolojia

Utafiti: Watu Wa Miaka 10 – 19 Wanapenda Sana Snapchat Na Instagram!

Utafiti: Watu Wa Miaka 10 – 19 Wanapenda Sana Snapchat Na Instagram!

Spread the love

Kwa mara ya kwanza mtandao wa Snapchat umeshika mioyo ya vijana haswa wale wa miaka 10 mpaka 19. Hapo awali mtandao wa Facebook ndio ulikuwa kila kitu. Kwa sasa utafiti unaonyesha hilo limebadilika

Utafiti huo ulihusisha vijana (10 – 19) 6,500 ambalo walionekana kuwa wanatumia na kuupenda sana mtandao huo. Aslimia 28 kati yao walitoa mawazo yao na kusema wao wanaona huo ndio mtandao wa kijamii ambao ni muhimu sana kuliko yote.

Snapchat Na Instagram Zikipambanishwa

Snapchat Na Instagram Zikipambanishwa

Instagram ilionekana ni muhimu sana kwa baadhi ya vijana ambao waliuchagua mtandao huo katika mitandao mingine yote. Instagram ilipata asilimia 27 kama mtandao muhimu sana, namba hii ikiwa ni nyuma ya Snapchat.

Katika utafiti uliopita vijana wengi (11 – 19) walisema mtandao wa Instagram ndio mtandao mzuri sana na ukashika alimia 33 wakati Snapchat ikishika asilimia 19 tuu.

Ukiangalia namba hizo utaona kuwa Snapchat imeweza kupanda kwa kasi sana. Kitu ambacho pia kionaonyesha mtandao huo unajitahidi katika kukuwa na kwamba wameuboresha mtandao huo sana

SOMA PIA  WhatsApp: Kupiga simu kwa njia ya sauti/video kwenye makundi inawezekana

Mtandao wa Snapchat tangia uanzishwa kwaka 2011 umeweza kuwapata zaidi ya watu milioni 100 kutembelea App yake. Uwezo wake wa kuwafikia zaidi vijana umeipa umaarufu mkubwa sana. Na kutokana na jambo hilo App hiyo imejikuta ikipata matangazo mengi.

Kutokana na Snapchat, asiliamia 60 ya watumiaji wake wa marekani ni vijana kati ya miaka 13 mpaka 34. Hata video za mtandao huo zinaangaliwa sana kwa siku. Mpaka sasa video zinaangaliwa mara bilioni 8 kwa siku.

Maelezo Ya Jinsi Ya Kutumia Mtandao Wa Snapchta Kwa Ufupi

Maelezo Ya Jinsi Ya Kutumia Mtandao Wa Snapchta Kwa Ufupi

Kwa sasa kampuni la Snapchat lina thamani ya dola bilioni 19 za kimarekani, namba hii inalifanya kampuni kuwa moja kati ya kampuni lenye thamani kubwa kati ya mitandao ya kijamii.

SOMA PIA  Facebook kuruhusu watumiaji wake kufuta kumbukumbu ya walichotafuta

Sifa hizo nyingi za Snapchat labda ndio zilizolifanya kampuni hilo kuwa na wapenzi wengi vijana.

Niandikie sehemu ya comment hapo chini hili wewe unalipokeaje? Je kw mtazamo wako huo ndio mtandao unaopendwa zaidi?. Pia usisite kuniambia mtandao wa kijamii ambao unakukosha zaidi. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania