Unaweza kufikiria kuwa makampuni yameweka kando kuhusu simu janja ambzo zinaweza kukunjika halikadhalika kukunjuka lakini la hasha! Kuna rununu nyingi tuu zitatoka katika kipindi cha majira ya joto mwaka huu.
Makampuni mbalimbali yamerudisha upya teknolojia ya simu ambazo zinakunjika nakukunjuka. Kampuni kama Oppo, Xiaomi, Vivo Samsung, ZTE zote hizi zina rununu ambazo zipo katika mtindo huu na kuna taarifa majira ya joto mwaka huu tutashuhudia zikitoka kwa wingi moja baada ya nyingine.
Samsung
Samsung ni moja ya makampuni ambayo yanatajwa kutoa simu janja zinazokunjika/kukunjuka ndani ya mwaka huu. Rununu zinazotajwa kuja katika majira ya joto ni Galaxy Z Flip 2 na Galaxy Z Fold 3 zote hizo zikitegemewa kutoka Julai 2021.

Oppo
Oppo nao wanatazamiwa kutoa simu janja ambayo ipo katika muundo wa kukunjika na kukunjuka. Mwaka 2020, walitoa maelezo ya jinsi Oppo X 2021 ilivyo japo kwa uchache ambapo wahusika waliishia kwa kusema simu hiyo ipo katika mtindo wa kuknjika/kukunjuka ingawa kampuni hiyo ilisemahaikuwa na mpango wa kuiingiza simu hiyo kwenye biashara.

Vivo
Habari za chini kwa chini zinasema Vivo nao wanatengeneza vsimu janja ya kukunjuka na kukunjika ambayo kioo chake kitakuwa na urefu wa inchi 7, ikikunjwa tunazungumzia urefu wa inchi 2.
Simu janja zote hizo zinatazamiwa kuzinduliwa wakati wa robo ya tatu ya mwaka 2021 na kuna mengi sana ambayo bado hayafahamiki hivyo kuwa na subira tu ndio kitu cha pekee kwa sasa mpaka hapo taarifa mpya zitakapopatikana.
Vyanzo: Android Authority, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.