Xiaomi bado wanaendeleza msururu wa simu janja na kuna taarifa kuwa Redmi Note 8 2021 ipo njiani kutoka mara baada ya miaka miwili kupita tangu mtangulizi wake kutoka.
Katika simu janja mojawapo ambayo inategemewa kutoka kwenye familia ya Redmi ni Note 8 ya mwaka 2021 na taayari baadhi ya sifa zinzoihusu simu hiyo zimeshafahamika wakati ambapo kampuni inafurahia kuuza simu janja takribani milioni 25 ya mtangulizi wake. Toleo hilo la Note 8 2021 linaelezwa kuwa na sifa hizi:
Urefu wa kioo|Kipuri mama
Simu janja husika inaelezwa kuwa ina kioo chenye urefu wa inchi 6.3 huku upande wa kipuri mama ni Helio G85 SoC ambayo inahusika kufanya ufanisi wa rununu uwe mzuri.
Kamera
Kampuni haisemi mengi kuhusu kamera kwenye simu janja ninayoizungumzia hapa lakini kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika rununu hii ina kamera nne huku ile kuu ikiwa na MP 48 ikifuatiwa na MP 8 na nyingine mbili zina MP 2. Kamera ya mbele ni moja tu na ina MP 13.
Uwezo wa betri|Mengineyo
Redmi Note 8 2021 inaelezwa kuwa na betri lenye 4000mAh, teknolojia ya kuchaji haraka ya 22.5W, itapatikana kwenye rangi mbili tu. Teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa kwa nyuma.
Ni wazi kuwa kuna mengi ambayo bado hajafahamika ya kuhusu simu janja husika ambayo inatazamiwa kutoka baadae mwaka huu ambayo inaaminika kuwa itafanana namtangulizi wake.
Vyanzo: GSMArena, Gadnwid
No Comment! Be the first one.