fbpx

Tanzania: Inashika nafasi ya 149 kwa kasi ya intaneti

0

Sambaza

Utafiti uliowekwa wazi unaonesha Tanzania imeporoka kiasi kwenye orodha ya mataifa mbalimbali yanapopangwa kwa sifa ya kasi ya intaneti.

Katika utafiti uliohusisha takriabni watumiaji milioni 160 duniani kote na ukihusisha mataifa 200 duniani kote umeonesha Tanzania inashika nafasi ya 149.

Singapore ndio taifa linaloshika namba moja ambapo kwa mtumiaji wa intaneti kudownload filamu ya GB 5 itamchukua wastani wa dakika 11 na sekunde 18 tuu kukamilisha, hii ni kwa wastani wa kasi ya intaneti ya Mbps 60.39.

kasi ya intaneti tanzania

Huduma ya intaneti imekuwa bora zaidi Tanzania kutokana na makampuni mengi zaidi kuzidi kuwekeza. Ila ukubwa wa nchi umekuwa changamoto kuhakikisha maboresho yanafanyika katika kila kona ya nchi

Kwa nafasi ya 149, Tanzania imeporomoka nafasi 10 ukilinganisha na mwaka jana, na kwa wastani itamchukua mtu saa 5, dakika 48 na sekunde 42 kushusha faili la GB 5.

Je, mataifa mengine ya Afrika Mashariki yanashika nafasi gani?

  • Uganda inashika nafasi ya 140, ikiwa imeporomoka nafasi 24 chini ukilinganisha na utafiti uliopita. Faili la video la GB 5 linachukua muda wa saa 4, dakika 45 na sekunde 45.
  • Rwanda inashika nafasi ya 130, ikiwa imeporomoka nafasi 13 chini ukilinganisha na ripoti ya mwisho. Faili la video la GB 5 llinachukua muda wa saa 4, dakika 19, na sekunde 4.
  • Kenya inaongoza kwa nchi za Afrika Mashariki, inashika nafasi ya 64, ikiwa imeporomoka nafasi 13. Faili la video la GB 5 linachukua muda wa saa moja, dakika 7 na sekunde 30.
  • Burundi inashika nafasi ya 134, hii ni mara ya kwanza imehusishwa kwenye utafiti huu. Faili la video la GB 5 linachukua muda wa saa 4, dakika 26, na sekunde 23.
INAYOHUSIANA  Bei ya Samsung Galaxy S10, S10 Plus na S0e Tanzania yatangazwa

Kwa kiasi kikubwa data hizi zinaweza zikawa vibaya kwa Tanzania kwa Afrika Mashariki kutokana na ukubwa wa nchi ukilinganisha na mataifa kama Rwanda na Burundi.

Kwa kiasi kikubwa kasi ya intaneti mijini imekuwa bora zaidi katika miaka ya hivi karibuni hapa nchini. Unaweza kudownload faili la GB 5 ndani ya lisaa moja hadi masaa 2 kupitia huduma mbalimbali nchini hasa hasa mijini.

Je, vipi wewe una mtazamo gani juu ya utafiti huu? Unakubaliana nao kwa data ya Tanzania? Angalia orodha nzima hapa chini.

Mataifa 16 ya juu, muda ni kwa mpangilio wa Saa: Dakika: Sekunde, itakayochukua faili la video la GB 5 kushushwa (download)

INAYOHUSIANA  Simu imepotea tuma IMEI kwenda cop@vsl.net - Hii habari ni ya uongo, usifanye hivyo

1. Singapore, Mbps 60.39, Muda 00:11:18

2. Sweden, Mbps 46.00, Muda 00:14:50

3. Denmark, Mbps 43.99, Muda 00:15:31

4. Norway, Mbps 40.12, Muda 00:17:01

5. Romania, Mbps 38.60, Muda 00:17:41

6. Ubeligiji, Mbps 36.71, Muda 00:18:36

7. Uholanzi (Netherlands), Mbps 35.95, Muda 00:18:59

8. Luxembourg, Mbps 35.14, Muda 00:19:26

9. Hungary, Mbps 34.01, Muda 00:20:04

10. Jersey, Mbps 30.90, Muda 00:22:06

11. Switzerland, Mbps 29.92, Muda 00:22:49

12. Japan, Mbps 28.94, Muda 00:23:35

13. Latvia, Mbps 28.63, Muda 00:23:51

14. Taiwan, Mbps 28.09, Muda 00:24:18

15. Estonia, Mbps 27.91, Muda 00:24:28

16. Uhispania, Mbps 27.19, Muda 00:25:06

Nafasi ya mwisho inashikiliwa na Yemen, ambapo ina wastani wa kasi ya Mbps 0.31, ambapo video ya GB 5 itachukua saa 36, dakika 52, na sekunde 20 kukamilika kuishusha.

Chanzo: Shirika la Cable la Uingereza – cable.co.uk

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.