fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu

Apps 10 Muhimu Kwa Ajili ya Simu za Nokia Asha

Apps 10 Muhimu Kwa Ajili ya Simu za Nokia Asha

Spread the love

nokia_asha_tanzania_appsSimu za Nokia Asha ni moja ya simu maarufu na zilizouzika zaidi kutoka Nokia kwa miaka yake ya mwishoni kabla ya kampuni hiyo kununuliwa na Microsoft na zinaendelea kuuzika vizuri ata baada ya kuwa chini ya Microsoft. Kwenye mipangilio ya familia za simu kulingana na uwezo wake kuna simu za kawaida, alafu kuna simu zinazoitwa ‘featured phones’ kisha zinafuata simu-janja (smartphones).

Simu za Nokia Asha nyingi zinaingia kwenye familia a ‘featured phones’, hii ikimaanisha ni simu zenye uwezo wa kiwango cha kawaida hii ikiwa ni pamoja na uwezo wa kupokea apps mpya, kutumia intaneti pamoja na mambo mengine mengi kama vile kuwa na kamera. Tofauti yake kubwa na simu-janja ni pamoja na kuwa simu-janja zinauwezo mkubwa zaidi wa kupokea apps zenye ukubwa zaidi na ata kiutendaji kazi zinakuwa na vitu kama RAM, prosesa na diski-uhifadhi wa kiwango cha juu zaidi kulinganisha na ‘featured phones’.

SOMA PIA  OnePlus 8T Pro kutoonekana tena mwaka huu

Ingawa familia ya simu za Nokia Asha zinawekwa kwenye kundi la ‘feautured’ bado inauwezo mzuri kwa matumizi ya kila siku ya kawaida, na kupitia ushirikiano na watengenezaji wa apps kuna apps mbalimbali zimetengenezwa kwa ajili ya simu hizi ili angalia kukufanya kutosononeka utamu wanaoupata watumiaji wa simu zenye Android au zile za iPhone kwa wingi apps walionao. Na hapa leo tumekuletea baadhi ya apps muhimu zaidi kuwa nazo kwa matumizi ya kawaida ya kila siku;

WhatsApp S40

WhatsApp ni moja ya app muhimu kabisa siku hizi kwa ajili ya mawasiliano. Hii inakuwezesha kuchati na marafiki wa nchini na nje ya nchi kwa uraisi kabisa, unaweza ipata kwa kubofya hapa – http://store.ovi.com/content/172049

CNN

Je unapenda kujua kinachotokea ulimwenguni kila siku? Ni muhimu!  Kupitia app ya CNN pata habari mbalimbali za ulimwenguni kupitia simu yako. Bofya kuipata – http://store.ovi.com/content/212837

Video HD

Je kuna video ya mwanamuziki mpya imetoka na upo mbali na kompyuta? App ya Video HD inakuwezesha kutazama video kutoka mtandao wa YouTube, tena kwa kiwango cha HD. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/161242

SOMA PIA  Simu za Samsung zinazouza kwa sana India - Samsung Galaxy J6 & J8

Editori PDF

Fungua na soma mafaili ya pdf kwa uraisi kwenye simu yako.  Kwa mafaili makubwa sana app hii inaweza chukua muda kidogo kuyafungua ila mwish0 wa huo muda utaweza kuyasoma kwa uzuri tuu. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/363956

Opera Mini Web Browser

Ulimwengu wa  simu za ‘featured’ ungekuwaje bila Opera Mini? Mgumu kweli kweli! Tokea enzi za miaka ile kabla simu janja hazijaenea na kuwa bei rahisi ni Opera Mini ndiyo ilikuwa inatusaidia kutumia mtandao, na inaendelea kubakia bora. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/46870

Sophie Cam

Je wewe unapenda kupiga picha? ”Viselfizi’ vya hapa na pale? Basi Sophie Cam itakufaa. Hii inakupa uwezo wa kubadilisha muonekano wa picha yako. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/212085

Wiki Encyclopedia

Kuelimika ni jambo zuri sana. Epuka kujikuta unaitaji kufahamu jambo flani kwa haraka alafu kuuliza kwa watu ni soo au upo peke yako, hapo ndio umuhimu wa app kama Encyclopedia unakuja. App hii inakusaidia kusaidia kufungua na kusoma mtandao maarufu wa WikiPedia kwa urahisi. Kuipakua –  http://store.ovi.com/content/202207

SOMA PIA  Kurudi kwa simu janja za BlackBerry na teknolojia ya 5G

Viber

Viber ni app nyingine maarufu duniani kwenye masuala ya kuchati. Viber inasifika kwa kukuwezesha ata kupigiana simu za bure na mwenzako anyetumia app hiyo. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/565945

Pocket Light Free

Umeme umezimika alafu hauna tochi? Giza nene? App hii inabadilisha kioo chako cha simu cha LED kuwa tochi pale unaitaji mwanga wa zaidi kuona kwenye giza. Kuipakua – http://store.ovi.com/content/289818

Facebook

Yes, mwishoni kabisa ni Facebook…hii haitaji maelezo mengi sana…Tunaielewa, ipakue kutoka hapa – http://store.ovi.com/content/238066

Kwa leo ni hapo tuu, je kuna jambo unataka lifahamu? Tuwasiliane kupitia akaunti zetu za Facebook, Twitter, Instagram au Google+ (Bofya kwenye jina kuungana nasi)

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania