Kampuni ya Microsoft imeamua kufanya toleo la programu maarufu ya uandishi ya MS Office kuwa bure kwenye simu na tableti zinazotumia programu uendeshaji za Android, iOS na Windwos OS. Wachambuzi mbalimbali wanachukulia uamuzi kuwa moja ya uamuzi mkubwa zaidi kuchukuliwa na kampuni hiyo.
Kabla ya uamuzi huu programu hizo zilikuwa zinakuruhusu kusoma lakini si kuweza kuchapa (kuandika) au kuboresha mafaili bila kujiandikisha katika mfumo wa malipo wao wa Office 365.
Kwa ufupi zaidi ni hivi;
- Kwa sasa tengeneza ‘document’/mafaili mapya bure na rekebisha mengine bure pia.
- Wametengeneza apps za kujitegemea za Word, Excel, na PowerPoint kwa ajili ya iPhone kufanana na zile za iPad.
- Apps za kujitegemea za Word, Excel na PowerPoint kwa ajili ya tableti za Android zipo njiani, za simu za Android zitafuata baada.
Bado hawajatoa tarehe rasmi ya kuja kwa apps za kujitegemea kwa Android kufanana na za iOS ila inategemewa kuwa hivi karibuni kwa sasa watumiaji wa mfumo wa Android wataendelea kupata huduma zote za Office kupitia app moja ya Microsoft Office inayopatikana kwenye soko la Google Play.
Kwa sasa unaweza shusha app ya Microsoft Office kwenye simu/tableti ya Android kwa kubofya hapa -> GooglePlay.
Watumiaji wa iPhone na iPad, bofya kushusha programu husika kutoka AppStore-> Word | Excel | PowerPoint
No Comment! Be the first one.