Microsoft mara kwa mara huwa wanaweka maboresho katika Windows zake, Maboresho hayo mara nyingi yanakuwa ni mazuri tuu, mimi binafsi hili nilimependa ila sasa…
Uzuti wake ni kwamba unaweza zima kukuiondoa kipengele hichi katika eneo la taskbar..
Kipengele hichi kipo spesheli katika windows 10 ili kukuletea habari mbalimbali duniani na pia bila kusahau kukugusia kuhusiana na hali ya hewa jinsi iivyo.
Kipengele hichi kinacho julikana kama “News and Interests” kimeanza kupatikana katika toleo la windows 10 kuanzia mwezi juni 2020.
Ni vigumu sana kuacha kukiona maana kikitokea tuu lazima uone na kinapatikana karibia na sehemu inapokaa tarehe na saa.
Ili kutaka kukiondoa sasa hebu ‘click’ eneo lolote katika ‘taskbar’
Ingia katika “News and Interests” na kisha zima kwa kuchagua ‘tun off’
Ukikamilisha kufanya hivyo tuu utashangaa kimeshatoka kabisa na utanendelea kutumia kompyuta yako kama kawaida.
Ukitaka kukirudisha siku yoyote fuata hatua hizo hizo na kisha chagua “Show Icon and Text.”
No Comment! Be the first one.