Nokia ambao wanaonekana kuendelea kujidhatiti kwenye ushindani wa kibiashara bado wanaona ni wakati sahihi wa kuwa na bidhaa kadha wa kadha; inayozungumzwa ni kuhusu Nokia 7.1 pamoja na machache yanayoihusu.
Kama tunavyojua kampuni fulani inapotaka kutoa bidhaa hasa za kidijiti panakuwepo, uvumi (taarifa kuvuja), n.k kuhusu kitu husika na pamekuwepo kuwa simu ijayo kutoka Nokia itaitwa “Nokia 7.1 Plus” lakini kutokana na taarifa za kuaminika simu hiyo haitakuwa ina maliziwa na neno “Plus” mwishoni.
Sasa simu hiyo itaitwaje?
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali imebainika kuwa simu hiyo ambayo inatazamiwa kutoka katika siku za usoni itwaiwa Nokia 7.1.
Toleo lijalo ni Nokia 7.1.
RAM/Diski uhifadhi.
Nokia wameamua kuifanya simu hiyo ambayo tunatazamia kuiona iktambulishwa ndani ya siku chache zijazo itakuwa na RAM GB 4 huku memori ya ndani ikiwa ni GB 64.
Moja ya kivutio kikubwa katika simu hiyo au bidhaa nyingine yoyote ni gharama yake ili mtu aweze kuinunua, bei yake inakadiriwa kuwa $463|Tsh. 1,064,900 rangi zikiwa ni Bluu na Chuma.
Kuhusu kuzinduliwa kwa simu hiyo ni tarehe za mwazoni mwa mwezi Oktoba 2018 na kama kawaida ya teknokona tutaleta undani wa sifa za simu husika mbele ya macho yenu.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|