fbpx
apps, Maujanja, Teknolojia, whatsapp

Ifanye app ya WhatsApp isichukue nafasi kubwa kwenye simu yako

ifanye-whatsapp-isichukue-nafasi-kubwa
Sambaza

Fahamu njia ya kuifanya WhatsApp isichukue nafasi kubwa kwenye simu yako ya android. Zuia mafaili kama picha n.k kuchukua nafasi kubwa kwenye simu yako.

Kwa watu wenye simu ambazo zina nafasi ndogo upande wa diski uhifadhi ninaamini wanapata changamoto ambayo inabidi wapunguze vitu kwenye simu ndio ipatikane nafasi ya kuongeza kwenye rununu.

Programu tumishi, WhatsApp ni moja ya vitu ambavyo vinachukua nafasi kubwa kwenye simu lakini tambua kuna njia ambayo unaweza ukaitumia kufanya kifaa husika kiwe na fasi ya kuridhisha:

Mosi, bofya kwenye zile nukta tatu zinazoziona upande wa kulia juu kwenye WhatsApp kisha nenda settings>>chats>>show media in gallery (ondoa alama ya pata).

WhatsApp isichukue nafasi
WhatsApp isichukue nafasi: Njia ya kutumia vitu vya kwenye WhatsApp kuonekana bila kuchukua nafasi kwenye memori ya ndani.

Pili, kwa vitu vinavyotumwa kwenye makundi pia inawezekana kutoviruhusu kuhifadhi kwenye simu kwa kuingia ndani ya kundi husika kisha kwenda kwenye kipengele cha “Group info” kutoka kwenye zile nukta tatu kisha utaondoa alama ya kukubali sehemu iliyoandikwa “Show media in gallery“.

Iwapo hutaki vitu vilivyotumwa na mtu fulani vionekane basi utabonenyeza picha ya mhusika kutoka kwenye uso wa mbele kwenye WhatsApp, bonyeza kwenye jina au namba ya mhusika kisha nenda moja kwa moja kwenye kipengele cha media na utachaua kutokukubali kwa vitu (picha/picha jongefu) alivyokutumia kwenye mfuko wa kuhifadhi.

nafasi kubwa
Njia mojawapo ya kuokoa nafasi kwenye memori ya ndani.

Hata kama simu yako ina nafasi kubwa lakini itafika kipindi itajaa na moja ya vitu ambavyo vitakuwa vimesababisha ni unavyotumiwa kwenye WhatsApp.

Suala hili halimaanishi utashindwa kuangalia kitu hicho tena la hasha! Lakini utakuwa unafungua kutokea kwenye programu husika.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kusafisha Kioo cha Laptop au TV
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|