Kama umegundua sasa hivi mitandao mingi ya kijamii imebadilisha kabisa mfumo wao wa kufanya biashara, Snapchat nayo haijabaki nyuma.
Kumbuka kuna kipindi mtandao huu ndio ulikua mtandao wa kijamii ambao unakua kwa kasi Zaidi ukilinganisha na mitandao mingine.
Kwa sasa mtandao umeona ni wakati sahihi wa kuanza kutambulisha huduma yake ya kulipia inayokwenda kwa jina la Snapchat Plus.
Kampuni imesema mpaka sasa imekua ikifanya majaribio ya ndani kwa ndani katika huduma hiyo mpya ya kulipia—hii inamaanisha itaachiwa hivi karibuni.
Bei ya huduma hii ya Snapchat Plus itategemeana na muda wa kifurusha yaaani cha mwezi ni takribani dola 4.84 za kimarekani na bei itakua inapungua kama mtu akichagua kifurushi cha nusu mwaka au mwaka mzima.
Vipengele vipya —ambavyo vitapatikana katika Snapchat Plus tuu — bado havijawekwa wazi kabisa kabisa lakini inasadikika uwezo wa kuweza ku’pin baadhi ya marafiki zako juu ya listi, uwezo wa kuwa na beji spesheli katika ukurasa wako.
Uwezo wa kuona ni marafiki wangapi wameangalia snap yako (zako) kwa mara nyingine tena, pia bila kusahau uwezo wa upendeleo katika huduma nyingi sana kama vile stika za aina yake.
Ni wazi kwa sasa mitandao mengi ya kijamii ina huduma za kulipia tumeshaanfika kuhisiana na Twitter Blue, WhatsApp Business Ya Kulipia, Telegram Premium na nyingine nyingi tuu
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Na utakua tayari kutumia snapchat ya kulipia?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.