fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Njia za Kufanya Malipo Mtandaoni
Spread the love

Uwepo wa biashara nyingi mtandaoni umepelekea kutengenezwa kwa njia mbalimbali za kufanya malipo mtandaoni. Njia hizi za malipo mtandaoni hutolewa na kampuni mbalimbali na mtumiaji anatakiwa kuwa na akaunti kwanza ili aweze kutumia huduma hizo.

Baadhi ya tovuti za biashara mtandaoni ni kama Amazon, Alibaba pamoja na Ebay, na unapotaka kununua bidhaa kupitia tovuti hizi utaletewa orodha ya njia za kutumia kukamilisha malipo yako. Orodha hiyo inakuwa na njia mbalimbali za malipo mtandaoni zinazoaminiwa katika tovuti hiyo. Njia hizo za malipo mtandaoni ni pamoja na:

PayPal: Ni moja kati ya njia z kufanya malipo mtandaoni yenye watuaji wengi kutoka nchi mbalimbali duniani. Paypal ni njia rahisi na salama kutumia katika ufayaji wa malipo mtandaoni. Pay pal wanatoa huduma zao kwa watu binafsi kupitia akaunti zao walizotengeneza na pia kwa wajasiriamali au makampuni ya biashara mtandaoni ambapo wanawapa ruhusa ya kuweka paypal kama njia ya kupokea malipo kutoka kwa wateja wao wa mtandaoni. Huduma hii ni ya kulipia kwa kukatwa kiasi cha hela kila unapofanya muamala.

SOMA PIA  Ajali ya Kwanza kusababishwa na Gari linalojiendesha la Google

Amazon Pay: Huu ni mfumo wa malipo ya mtandaoni unaomilikiwa na kampuni ya Amazon. Mfumo huu unaweza kutumiwa na wateja, wauzaji wa Amazon pamoja na tovuti zingine za kibiashara mtandaoni. Katika mfumo huu mteja anapokuwa na akaunti hatasumbuka tena kujaza taarifa zake anapotaka kununua bidhaa badala yake atabonyeza tu kitufe cha kumruhusu kulipia kwa mfumo huu na kuendelea na hatua zingine. Pia kuna makato katika huduma hii ambayo ni 2.9% kwa kila muamala unaofanyika.

Njia za Kufanya Malipo Mtandaoni

Picha: Mteja akifanya malipo mtandaoni

Google Pay: Ni mfumo wa kufanya malipo mtandaoni kidigitali uliotengenezwa na Google. Mfumo huu unamuwezesha mtu kujaza taarifa za kadi yake ya benki ili aweze kufanya malipo ya huduma za mtandaoni kwa wepesi zaidi kupitia mfumo huu wa Google. Pia kupitia mfumo huu mtumiaji hatalazimika kujaza taarifa zake binafsi kila anapotaka kulipia huduma mtandaoni badala yake atatumia mfumo huu. Huduma hii ya Google inatolewa bure kwa pande zote yaani kwa mnunuaji na pia muuzaji wa bidhaa au mtoa huduma.

SOMA PIA  Google kupigwa faini ya kuvunja rekodi barani Ulaya

Apple Pay: Apple pia inatoa huduma za malipo mtandaoni kupitia programu yake ya Apple pay inayopatikana kwenye vifaa vyao vyote vya kielektroniki kama iPhone na Apple watch. Programu hiyo inakuja na kifaa chako na hautaweza kuipakua kutoka sehemu yoyote ile. Huduma hii pia inamhitaji mtumiaji kujaza taarifa za akaunti yake ya benki ili aweze kufanya malipo mtandaoni kupitia huduma hii. Apple wanatoa huduma hii bure kwa pande zote mlipia huduma na mtoa huduma za mtandaoni.

SOMA PIA  Gemu la Snake (Nyoka) Linakuja Kwenye Simu Janja

Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kujifunza mambo mbalimbali kuhusu teknolojia na matumizi yake. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania