fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Ndege Teknolojia Uchambuzi

Fahamu kuhusu Ndege ya Concorde

Fahamu kuhusu Ndege ya Concorde
Spread the love

Concorde ilikuwa ni ndege ya abiria yenye uwezo mkubwa wa spidi kushinda hata spidi ya sauti. Ndege hii ilitengenezwa na kampuni ya British Aircraft Corporation (BAC) ikishirikiana na kampuni zingine na ilitumiwa na Mashirika mawili tu ya ndege ambayo ni British Airways pamoja na Air France. Concorde ilikuwa na spidi ya kwenda 2180 km kwa lisaa.

Ndege ya Concorde ilitengenezwa na kuanza kutumika mwaka 1976 na ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 92 mpaka 128. Concorde ilifanya kazi miaka 27 tu na kuacha kutumika mwaka 2003. Ndege hii ya Concorde ilikuwa ni moja kati ya ndege mbili tu pekee zenye uwezo huo mkubwa wa spidi nyingine ilikuwa ni ndege kutoka Russia iliyoitwa Tupolev Tu-144.

SOMA PIA  Ijue Hot Knot; Sahau Kutuma Mafaili kwa Teknolojia ya Bluetooth, hii ni Bora Zaidi

Kuna sababu mbalimbali zilizopelekea ndege ya Concorde kuacha kutumika kabisa, sababu hizo ni pamoja na Gharama za uendeshaji zilikuwa ni kubwa mno kutokana na teknolojia iliyokuwa ikitumiaka katika ndege hiyo, Ajali iliyotokea mwaka 2000 iliyosababisha watu kuogopa kupanda ndege hiyo na hivyo kupungukiwa abiria kwa kipindi kirefu na pia Kero ya sauti ambapo baadhi ya nchi zilikataa Concorde kutua katika viwanja vyake kutokana na kuwa na sauti kubwa mno inapotembea.

Ndege ya Concorde

Picha: Muonekano wa Concorde ikiwa inatua Uwaja wa ndege.

Ndege ya Concorde ilitumia injini nne ambazo zilitengenezwa na kampuni ya Rolls Royce. Safari yenye spidi kuliko zote iliyofanyika na ndege hii ni ya mwaka 1996 ambapo ilitumia masaa 2, dakika 52 na sekund 59 kutoka New York mpaka London. Kwa maelezo ya undani zaidi soma hapa.

SOMA PIA  Teknolojia ya FaceID kwenye iPhone X 'yamvuruga' John Cena

Endelea kutembelea tovuti yetu uweze kufahamu zaidi kuhusu teknolojia mbalimbali. Pia usiache kututafuta katika mitandao ya kijamii uweze kupata taarifa tunapochapisha makala mpya. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania