NASA ni shirika la kitaifa la Utawala wa Anga nchini Marekani linalohusika na utafiti pamoja na utengenezaji wa teknolojia za Anga. Shirika hili la NASA lilianzishwa maalum kwaajili ya kusimamia mambo makuu manne ikiwemo kufanya tafiti kuhusu chimbuko la dunia pamoja na sayari zingine na Kutengeneza teknolojia za kumwezesha binadamu kufanya utafiti wa kisanyansi nje ya dunia.
Shirika la NASA lilianzishwa mwaka 1957 na makao makuu ya shirika hili yapo Washington DC Marekani. Tangu kuanzishwa kwake shirika hili limekuwa likiendesha programu mbalimbali za utafiti wa Anga ikiwemo Apollo, Viking, Mariner, Voyager na Galileo. Pia shirika hilo limehusika na utengenezaji wa vyombo maalum kwaajili ya kusafiria nje ya dunia kama Apollo 11.
Programu ya Apollo ndo programu kubwa iliyoipa sifa shirika la NASA kwasababu programu hiyo ilihusu kupeleka binadamu kwenye mwezi kwa mara ya kwanza. Mwaka 1969 nchi ya Marekani ilifanikiwa kupeleka binadamu kwa mara ya kwanza mwezini kupitia chombo cha Apollo 11. Pia programu ya Viking ilihusu kupeleka roboti katika sayari ya Mars na kutuma picha za mazingira ya sayari hiyo.
Kutokana na kufanikiwa kwa programu ya Apollo kupeleka binadamu mwezini na kurudi salama, Mafanikio ya programu hii yaliwezesha shirika la NASA kuendeleza programu zingine na pia kuanzisha uhusiano wa kimataifa na nchi zingine kwaajili ya kushirikiana katika uboreshaji wa teknolojia za anga. Pia programu zingine za NASA kama Viking, Mariner, Voyager na Galileo zilihusisha kutumwa kwa maroboti nje ya dunia kwenda kufanya uchunguzi katika sayari zingine pamoja na kutuma picha ya mazingira ya huko.
No Comment! Be the first one.