fbpx

Facebook, instagram, Mtandao wa Kijamii, Teknolojia

Watumiaji wa Instagram wamekuwa wakichunguliwa kupitia kamera za iPhone

watumiaji-wa-instagram-wamekuwa-wakichunguliwa-kupitia-kamera-za-iphone

Sambaza

Watumiaji wengi wa simu janja duniani kote mitandao ya kijamii ambayo ina watumiaji wengi wa kila siku inajumuisha Facebook, Instagram na nyinginezo ni WhatsApp, Twitter lakini sasa mtandao mkubwa wa kijamii umelalamikiwa!.

Mitandao ya kijamii imekuwa chanzo cha mapato kwa baadhi ya watumiaji na kuifanya kuwa maarufu huku ikisaidia kubadilisha maisha ya watu. Katika ukuaji wa teknolojia na uwepo wa simu janja inaweza kuwa vigumu kwa baadhi ya watu kumaliza siku bila kutembelea mitandao ya kijamii. Na hilli linakuwa ni kwa sababu ya uraibu au mambo mengine tuu.

Sasa kutokana na utandawazi na wengi wetu tunatumia mitandao ya kijamii tufahamu hili: Facebook imelalamikiwa kwa kusemekana imekuwa ikiwaangalia watumiaji wa Instagram kupitia kamera ya simu. Inakuaje?

Mwezi Julai mwaka huu Instagram ilikuwa inaona watumiaji wake wanaotumia iPhone wakati ambao mtu alikuwa hatumii kamera. Jambo ambalo liliweza kufanya Facebook kuweza kuona faragha ya ndani kabisa kama madhari yamtu anapoishi bila ya mhusika kujua.

watumiaji wa Instagram
Mwezi uliopita Facebook ililalamikiwa kutumia teknolojia ya kutambua uso kukusanya taarifa za mtu kwa maslahu yao binafsi.

Malamiko hayo Facebook imeyakataa na kusema ni tatizo tuu la programu tumishi husika (Instagram) kupeleka taarifa fupi kuwa kamera ya kwenye iPhone ilikuwa ikitumika na wakati si kweli.

Facebook wanasema tayari tatizo hilo linashugulikiwa kuweka mambo sawa. Iwapo kitendo hicho kilifanyika kweli basi hatuna budi kuwa makini sana kwa chochote tunachokifanya kwenye mitandao ya kijamii.

Waswahili husema “Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja”. Endelea kutufuatilia kila uchwao kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.

Vyanzo: Gadgets 360, Bloomberg.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*