Pata picha huduma ya WhatsApp Business ikiwa ni ya kulipia, unahisi ni vipengele gani ambavyo vitaongezwa ili kuendana na hali halisi ya malipo hayo?.
Kwa haraka haraka hapa ni lazima kwa mtandao huo kuweza kuongeza vipengele ambavyo havipo katika App ya kawaida ya WhatsApp Business.

Kipengele hiki kinapewa jina la WhatsApp Premium, na kwa haraka haraka inasemekana kitakua kinapatikana katika WhatsApp Business ya kawaida.
Kipengele Hichi Kitakua Na Uwezo Wa Kufanya Yafuatayo.
- Uwezo wa kuunganisha hadi vifaa kumi kwa kutumia namba (moja) hiyo hiyo.
- Pia Hata uwezo wa kuvipa majina vifaa hivyo itakua ni juu ya mtu –namba bado itabaki ile ile –na kifaa
- Uwezo wa kujitengenezea link ya chaguo lako (kwa wafanya biashara), link zitatumika kuwapeleka wateja moja kwa moja kwenye uwanja wa meseji katika WhatsApp ya mfanya biashara.
Kwa haraka haraka ni kwamba vipengele hivi ni vipya kabisa kwa kwenye WhatsApp business ya kawaida haviwezi kufanyika kabisa.

Maboresho katika mtandoa wa WhatsApp ni mengi sana hivi kairibuni ili kujihakikishia kuwa umeyapitia yote hebu pitia >>HAPA<<
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Je Uko Tayari Kutua Kiasi Cha Pesa Ili Uwezo Kupata Huduma Hizo Tajwa (Pengine Baadae Ziataongezwa)?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.