fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao wa Kijamii Twitter

FAHAMU ‘Twitter Blue’ Ni Nini!

FAHAMU ‘Twitter Blue’ Ni Nini!

Spread the love

Umeshawahi kusikia kuhusiana na Twitter Blue? ushawahi kufikiria kulipia ili kutumia mtandao wa kijamii? endelea nasi ili tukujuze kuhusiana na twitter blue.

Twitter ni sawa na mtandao (App) ya twitter ya kawaida tuu ila inakua imeongezewa vipengele ambavyo vitakusisimua tuu wakati unatumia mtandao huo

Twitter Blue Ina Vipengele Hivi

Hifadhi Tweet (Bookmarks Folder)

Kipengele Cha Bookmark Ndani Ya Twitter Blue

Kipengele Cha Bookmark Ndani Ya Twitter Blue

Kipengele hichi ni kama kile cha twitter kawaida kinachoitwa ‘bookmark’ na kinakuwezesha kuhifadhi (save) Tweets zako zote ubaya wake ni kwamba ulikua huwezi kutafuta (search) tweet hizo lakini kwa twitter blue ni kwamba kuna ‘folder’ kabisa limewekwa na unaweza tafuta tweet moja moja.

Unaweza ukatengeneza mafaili (folder) mengi sana na kisa unaweza ukachakua usave kitu kwenye folder gani… unaweza badilisha jina na hata rangi ya mafaili hayo.

SOMA PIA  Hisia ya Vita ya Gaza Duniani

Rekebisha Tweet (Undo Tweet)

Kipengele Cha 'Undo' Ndani Ya Twitter Blue

Kipengele Cha ‘Undo’ Ndani Ya Twitter Blue

Tumeshazoea hii ya kutuma tweet alafu tunakuambuka tumefanya makosa labda ya kiuandishi ila kuepukana na hili tunaamua kufuta tweet yote na kutuma nyingine.

Hii uzuri wake ni kwamba inakuja na batani ya ‘Undo’ ambayo kazi yake kubwa itakufanya kuweza kurekebisha tweet bila ya kuifuta yote kama ilivyokua mwanzo.

Hii itakua inafanya kazi sekunde 30 baada ya kutuma tweet yako kwani ndani ya muda huo ndio unaweza badalisha tweet hiyo. ubaya wake ni kwamba kama tweet hiyo itakua imeshaenda kwa followers wako basi hapo huna budi itabidi kufuta na kutuma nyingine mpya kama zamani.

SOMA PIA  "Unaweza Nisikia ....?" - Snowden Ajiunga Twitter

Soma Tweet Ndefu Kwa Mara Moja (Reader Mode)

Kipengele Cha 'Reader Mode' Ndani Ya Twitter Blue

Kipengele Cha ‘Reader Mode’ Ndani Ya Twitter Blue

Ni jambo la kwaida kabisa kupitia mtandao wa twitter kuandika tweet fupi fupi nyingi zenye dhima ya kuelezea kitu kimoja maarufu kama ‘thread’ lakini ni wazi kusoma zote saa nyingine itakua sio  poa!

Inakuja na kipengele cha ‘Read More’ (Reader mode) ambapo hapo utaweza kuona Tweet yote hata kama ni ndefu sana.

Badilisha Mandhari (Themes)

Unaweza kubadilisha madhari na rangi katika Twitter Blue. Hii inamaana unaweza kubadilisha madhari ile ya kawaida ambayo umeizoea katika Twitter ya kawaida.

Huduma Kwa Wateja Kwa Ukaribu Zaidi (Twitter Support)

Huduma kwa wateja katika twitter Blue ni ya ukaribu zaidi kuliko twitter ya kawaida. Ni wazi nadhani anaetoa hela itabidi ajaliwe zaidi kuliko yule ambae hatoi.

SOMA PIA  m.facebook.com kuondolewa uwezo wa kuchati, lazima kutumia Facebook Messenger

Hii inaanisha kuwa huduma kwa wateja itakua ya karibu zaidi na ya uharaka lakini vigezo na masharti vitazingatiwa kwani mambo kama lugha chafu havitakua na nafasi.

Jinsi Ya Kujiunga Na Twitter Blue

Ingia katika mistari mitatu katika App ya twitter na kisha chagua Twitter Blue na fuata maelekezo

Mistari Mitatu Katika App Ya Twitter

Mistari Mitatu Katika App Ya Twitter

Habari zilizopo ni kwamba mpaka sasa twitter blue imeachiwa kwa baadhi ya maeneo tuu na inagharimu dola 3 kwa mwezi. Swali lililopo ni kwamba je unaweza kulipia kiasi hicho ili kupata huduma za ziada hapo juu?

Kama Twitter blue kwako bado huwezi kuipata basi itabidi usubirie maana bado haijafika sehemu nyingi.

Ningependa kusikia kutoka kwako, hili limiekaaje? niandikie hapo chini katika eneo la comment

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania