Teknolojia inayohusisha simu za kujikunja inaonekana kurudi kwa kasi shuhuda zikionekana kwa makampuni makubwa kama Samsung, Motorola, Oppo, Xiaomi, Google, n.k wakirudisha bidhaa za aina hiyo kwenye macho ya watu baada ya kupotea kwa karibu miongo miwili.
Mwishoni mwa mwaka 2020 zilikuwepo ripoti kuwa Samsung itatengeneza vioo vyenye uwezo kukunjuka na kukunjuka kwa ajili ya Vivo, Oppo, Google, Xiaomi. Taarifa hizo zimezidi kupewa uzito wake kwani ukiacha Vivo kuna viasharia kuwa Samsung itahusika vyema kutengeneza vioo ambavyo vinakujnika/kukunjuka vitavyowekwa kwenye simu janja wanazotarajia kuzitoa.
Kuna taarifa za kuaminika kuwa Samsung inatengeneza kioo cha ubora wa OLED chenye inchi 7.6 ambacho kina uwezo wa kukunjika na kukunjuka kwa ajili ya simu za mkunjo kutoka Google.
Xiaomi
Taarifa zinasema kuwa Xiaomi inabadili mtindo kutoka kwenye vioo vya kukunjuka kwa nje hadi kwenye mtindo wa kukunjika kwa ndani ambapo wanatazamiwa kushikiana na Samsung lakini pia CSOT. Kioo hicho kinategemewa kuwa na urefu wa inchi 8.02 kikikunjuliwa, urefu wa ichi 6.38 kikikunjwa.
Oppo
Kwa mujibu wa taarifa wao Oppo vioo yao vutakuwa vinakunjuka kutoka juu kwenda chini hivyo ukubwa wa kioo cha nje inapokunjwa unakadiriwa kuwa na urefu inchi 1.5 hadi inchi 2 huku ikikunjuliwa kioo hicho kinategemewa kuwa kirefu zaidi endapo kitakunjuliwa.
Hakika kama waswahili wasemavyo kuwa “Vya kale dhahabu” ndivyo hivyo tunavyozidi kuona makampuni yakishirikiana kurudisha teknolojia iliyokuwa imetoweka (vioo vya kujikunja na kukunjuka) kwa miaka mingi katika hali ya usasa kulingana na mabadiliko ya teknolojia.
Vyanzo: Android Authority, GSMArena
One Comment