Mwaka 2020 ulikuwa wenye changamoto nyingi tuu za kiuchumi duniani kote lakini hata hivyo mambo yaliendelea na bado yanaendelea kusonga na kwa mujibu wa takwimuu zilizotoka Apple ndio kinara wa mauzo kwenye robo ya mwisho ya mwaka uliopita.
Wakati dunia inapitia katika kipindi kigumu lakini kwa wengine ni furaha kwa kuweza kufanya vizuri kwenye soko la ushindani wa bidhaa za kidijiti kutokana na kuuza zaidi kuliko wengine. Simu janja za Apple, Samsung na Xiaomi ndio zipo kwenye 10 bora; Apple ilikuwa na rununu 5, Samsung-4 na Xiaomi-1. Mchanganuo wake ni kama ifuatavyo:-
Simu janja zilizouzika zaidi mwaka 2020
Simu janja | Idadi | Wastani wa bei kwa simu moja |
iPhone 11 | 64.8 milioni | $754 |
iPhone SE (2020) | 24.2 milioni | $451 |
iPhone 12 | 23.3 milioni | $896 |
Samsung Galaxy A51 | 23.2 milioni | $269 |
Samsung Galaxy A21s | 19.4 milioni | $192 |
Samsung Galaxy A01 | 16.9 milioni | $115 |
iPhone 12 Pro Max | 16.8 milioni | $1,232 |
Samsung Galaxy A11 | 15.3 milioni | $158 |
Redmi Note 9 Pro | 15 milioni | $161 |
iPhone 12 Mini | 14.8 milioni | $796 |
iPhone 12 Pro ndio rununu ya pekee kutoka kwenye familia ya toleo la 12 kutokuwepo kwenye orodha ya 10 bora. Ulikuwa mwaka wa neema kwa Apple hususani mauzo ya iPhone 11 ambapo kwa miaka kadhaa nafasi ya kwanza ilikuwa ikishikiliwa na Samsung.
Je, wewe unamiliki mojawapo ya simu zilizoingia kwenye kumi bora?
Chanzo: Gadgets 360
No Comment! Be the first one.