fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti Teknolojia

Rekodi mpya kuhusu kasi ya intaneti

Hivi karibuni imetoka rekodi mpya inayohusu kasi ya intaneti na dunia ya leo furaha ya watu ni kutumia intaneti yenye kasi kitu ambacho kitawezesha kushusha kitu kutoka mtandaoni kwa kutumia muda mfupi.

Teknolojia ya kutumia nyanya za Fiber inaonekana kubadilisha kabisa kasi ya intaneti tangu hapo ilipoanza kutumiwa mwaka 1988 ambapo ilitumiwa kuungaanisha Marekani na bara la Ulaya kimawasiliano. Tangu wakati huo matumizi ya teknolojia hiyo yamekuwa yakiwa kwa kasi sana na kuvutia wengi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ufanisi, gharama, n.k.

Rekodi mpya

Nyanya za Fiber ni nyembamba sana, zenye uwezo wa kusafirisha mawasiliano kwa haraka zaidi kulinganisha na miundombinu mingine.

Kwa ushirikiano wa kampuni mbili, Xtera na KDDI Research walirekodi kasi zaidi ya mtandao. kasi ya 178 TPBS (Terabits per Second) kwa maana ya kwamba kuweza kushusha kila filamu na sinema zote kwenye Netflix chini ya sekunde moja. Jambo hilo lilifanikiwa baada ya timu ya watafiti kutoka kampuni zote mbili  iliyoongozwa na Dkt. Lidia Galdino kutumia uwanja mpana zaidi kusafirisha data ambapo wengi hutumia kati ya 4.5THz na 9THz wakati wao waliamua kwenda hadi 16.8THz.

Rekodi mpya

Dkt. Lidia Galdino kutoka UCL Electronic & Electrical Engineering aliyeongoza timu ya wataalamu walioweza kurekodi kasi kubwa zaidi ya intaneti.

kwa kasi hii mpya ni inashika nafasi ya tano kwa kasi zaidi kulinganisha na iliyo iliyopita iliyokuwa imerekodiwa na timu huko Japan. Haya tuambie kwenye eneo ulipo kasi ya intaneti inasoma ngapi? BOFYA HAPA kuweza kujua.

Chanzo: SciTechDaily

SOMA PIA  Uwezo wa kuhama mtandao wa simu bila ya kubadili laini: Vitu muhimu vya kufahamu
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania