Magemu ya kwenye Android polepole yaanza kufanyiwa majaribio hivyo kufanya wale ambao wanapenda aina hiyo ya burudani kuweza kuipata kwenye kompyuta zao zinazotumia Windows.
Hivi sasa kuna Windows 11 na wakati programu hiyo endeshi inazinduliwa wahusika waliahidi kuwa magemu ya Android yatapelekwa huko kitu ambacho kimeshaanza kuonekana lakini si kwenye toleo hilo jipya tu bali hata baadhi ya kompyuta zinazotumia Windows 10 wanaweza kucheza magemu hayo yanayopatikana kwenye Android.
Je, ni kompyuta zote tuu zenye Windows 10/11 zina uwezo wa kukubali aina hiyo ya kichangamsha akili?
Ni muhimu kufahamu kuwa unapozungumzia mtu kucheza magemu kwenye kompyuta basi ni lazima kifaa hicho husika kiwe na sifa ambazo hazitaathiri ufanisi wake kazi nyingine kwenye kipakataalishi au zile za mezani. Kimsingi vichangamsha hivi ya akili kwenye Android ili kucheza kwenye kompyuta zenye Windows 10/11 basi angalau zinatakiwa ziwe na sifa hizi:
- kuwa na toleo la karibuni kabisa la Windows 10 au 11,
- kipuri mama (CPU) iwe ya Octa core halikadhalika upande wa ubora wa picha (GPU) iwe yenye nguvu uwezo wa kati au zaidi,
- memori-RAM ni GB 8 na diski uhifadhi ianzie angalau 20 GB SSD.
Mojwapo ya gemu unaloweza kucheza kwenye Android halikadhalika Windows 10/11.
Asphalt 9, Gardenscapes na Homescapes yameshaanza kupatikana kwenye Windows 10/11 kwa baadhi ya nchi. Je, wewe msomaji wetu kompyuta unayoitumia ina sifa za kuweza kufurahia hayo na mengineyo ya “Kileo”?
Vyanzo: GSMArena, mitandao mingine
No Comment! Be the first one.