fbpx

Matangazo kwenye WhatsApp Status yapo njiani kuja 2020

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Je utafurahia kuwepo kwa matangazo kwenye WhatsApp Status? Katika apps zote za mtandao wa kijamii chini ya umiliki wa Facebook ni app ya WhatsApp tuu ndio ilikuwa bado haijawekwa matangazo. Baada ya uvumi wa muda mrefu sasa taarifa ni rasmi, matangazo yanakuja.

Katika apps zote za kimatandao ya kijamii chini ya umiliki wa Facebook ni WhatsApp tuu ndio ilikuwa bado haina matangazo ndani yake. Sasa inasemakana kufikia mwaka 2020 app hiyo itakuwa na matangazo pia.

Matangazo kwenye WhatsApp Status yanakuja 2020.

Matangazo kwenye WhatsApp Status yanakuja 2020.

  • Hii inatokana na imani ya muda mrefu ya waanzilishi wa huduma ya WhatsApp. Walikuwa na msimamo imara dhidi ya matangazo kwenye huduma hiyo, kwao ilikuwa ni bora ata kuleta huduma ya kulipia kwa gharama ndogo ili tu kuepusha matangazo kwenye app hiyo.
  • Katika makubaliano yao na Facebook wakati wanakubali kunuliliwa na Facebook mwaka 2014 ilikuwa pia ni kuwa Facebook wasije kuweka matangazo kwenye huduma hiyo. Inasemakana Facebook, chini ya Mark Zuckerberg walikubali ila hivi karibuni walibadilika na kusema lazima waanzishe huduma ya matangazo ndani ya app hii maarufu. Suala hili tayari limewafanya waanzilishi wa huduma kujitoa kwenye kampuni hiyo na kuongea vikali dhidi ya Facebook – ikiwa ni pamoja na kusisitiza watumiaji wafanye uamuzi wa kufuta apps za Facebook.
INAYOHUSIANA  Kundi la wadukuzi latishia kufanya Pokémon Go kuwa offline Agosti 1

Katika kongamano na watengenezaji wa huduma za intaneti (developers) Facebook wametambulisha mfumo wa matangazo yatakayokuja hivi karibuni katika app ya WhatsApp.

Matangazo yatakuwaje?

matangazo kwenye whatsapp status

Matangazo yatakuwa kwenye Facebook, Instagram na WhatsApp Status

  • Kutakuwa na matangazo kwa ajili ya apps za Instagram na Facebook ambayo mtu akibofya/click atapelekwa kwenye app ya WhatsApp. Hii itakuwa nzuri kwa makampuni kuweza kuchati moja kwa moja na wateja wao.
  • Matangazo ya ndani ya WhatsApp wataanza na matangazo katika eneo la Stories. WhatsApp stories inatumiwa na mamilioni ya watu kila siku
INAYOHUSIANA  Apigwa faini milioni 9 kwa kubonyeza kitufe cha 'Like' facebook

Watumiaji wengi wamepokea habari hiyo kwa hasira, hadi sasa kuna comments nyingi mtandaoni wakitishia kuachana na app hiyo na kuhamia kwenye app ya Telegram kama Facebook ataleta matangazo kwenye app ya WhatsApp.

Ili Facebook aweze kuhakikisha matangazo yanawafikia watu sahihi ina maana kutakuwa na utumiaji wa data za watumiaji wa app hii maarufu. Swali kwa wengi je Facebook watatumia data gani kufanikisha hili – je itakuwa na aina ya Status unazopost au mazungumzo unayofanya? Haijalishi Facebook atatoa uhakika wa aina gani, bado watumiaji wengi hawana imani na Facebook pale linapokuja suala la utumiaji wa data kwa ajili ya matangazo.

INAYOHUSIANA  WhatsApp yaleta kipengele kipya kwenye makundi #Masasisho

Je wewe una mtazamo gani na ujio wa matangazo? Je kati ya kupata matangazo au kulipia huduma ya WhatsApp, kipi unaona ni bora?

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.