Instagram ni moja ya mtandao wa kijamii ambao una watumiaji wengi zaidi duniani na kila leo inazidi kuongeza wateja wapya ambao wanafungua akaunti huko. Tunafamu vyema kile kitufe cha “Subscribe” kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii sasa kimefika Instagram!
Mara kwa mara Instaagram imekuwa ikiboreshwa kwa lengo la kuifanya iwe na mvuto wa kipekee hivyo kuzidi kufarahisha wateja wake halikadhalika kupata na wengine wapya pia. Katika siku za karibuni watumiaji wa Instagram nchini Marekani ambao wapo kwenye kundi la waundaji kwa tafsiri isiyo rasmi ama “Creators” wanaona kitufe cha “Subscribe” kwenye akaunti zao.
Kwanini kitufe hicho kimepelekwa huko?
Mwezi Juni 2020, Facebook iliweka kitufe hicho ndani ya mtandao huo wa kijamii kwa lengo la kusaidia “Waundaji” waweze kujitengenezea pesa. Sababu hiyohiyo ndio ilifanya kitufe cha “Subscribe” kwenye akaunti za walengwa. Sisi ambao tutapenda kupata taarifa moto moto za waundaji ndani ya Instagram itatulazimu kubofya kitufe husika ili kuweza kupata taarifa mara tu wanapopandisha kitu hewani.
Kwa upande wa waundaji kwenye Instagram wanaweza kutumia vipengele vya Insta Live, Stories na Badges kuweka vitu mahususi kwa ajili ya watu wanaowafuatilia na kulipia kuweza kupata habari kwa kile ambacho amekipsndisha hewani kupitia sehemu husika.
Waundaji watakuwa na uwezo wa kuruhusu kitufe hicho kipya kwenye akaunti zao na kuweka kiwango cha ada ya kila mwezi watakayotaka wao 🙄 🙄 lakini Instagram haianza kuwalipisha watu kuweza kupata huduma hiyo hadi mwezi Juni 2023 😆 😆 .
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.