fbpx

Zlatan Ibrahimovic azindua game yake mpya ya Zlatan Legends

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mchezaji nyota wa mpira wa miguu wa Sweden Ibrahimovic Zlatan amezindua mchezo (game) wake mpya wa utakaojulikana kwa jina la Zlatan Legends.

Jumanne wiki hii lilitolewa tangazo la video fupi linalohusu game hilo la michezo ya kupigana. Kampuni ya Kiswideni ya ISBT GAMES ndio wahusika wa utayarishaji wa mchezo huo unaotarajiwa kuanza kupatikana tarehe 17 ya Agosti mwaka huu.

Zlatan Ibrahimovic legends app

Zlatan Ibrahimovic

Zlatan Ibrahimovic: Zlatan Legends

Game hiyo iliyotengenezwa kwa miaka miwili, itapatikana katika Simu Janja, na Simu za mfumo wa iOS ndio zitaanza kupata mchezo huo na kisha kufuatiwa na simu za mfumo wa Android.

INAYOHUSIANA  Tuma na Pokea SMS kwenye Kompyuta yako

Katika video fupi ya tangazo la mchezo huo inasikika sauti ya Ibrahimovic akisema, “Nilidhani hapakuwa na changamoto zilizobakia. Ndivyo walivyokuja. Mchezo mpya, sheria mpya na mpinzani mpya. Mtu ninayemjua vizuri sana. Katika Siku hii ulimwengu utajua kwamba kuna Zlatan mmoja tu.”

Zlatan Ibrahimovic

Baada ya maneno hayo anaoneshwa mtu mwenye taswira kama ya Ibrahimovic akiwa amevaa mavazi
ya suti za mapigano huku ametanua mikono yake kwa namna ile ile inayotumiwa na mchezaji huyo anaposhangilia pindi afungapo goli.

INAYOHUSIANA  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Kwa sasa mchezaji huyo hana timu anayoichezea baada ya kufanyiwa oparesheni ya mguu kutokana kuumia katika mechi akiwa na timu ya Manchester Unite ya Uingereza. Mkataba wake wa mwaka mmoja na Man U umekwisha.

Licha ya usajili wa bei kubwa wa mshambuliaji Romeo Lukaku lakini kuna taarifa kwamba Kocha wa Man United, Jose Mourinho ana mpango wa kumpa mkataba mwingine Zlatan kuisaidia timu hiyo kutwaa vikombe.

INAYOHUSIANA  Instagram Waanza Kutuma Barua Pepe za 'Mambo Muhimu'

Zlatan amechezea klabu kubwa na kupata mafanikio kote alipopita anaamini ukimtoa Mchezaji Lionel Messi ni yeye ndiye anafaa kuwa gwiji wa mchezo huo duniani.

Maoni ya wasomaji wengi yameonesha kuwa na hamu ya kuuona mchezo huo wa Zlatan Legends pindi utakapoanza kupatikana katika Play Store na Apple Store. Bado haijajulikana mchezo huo utakuwa wa bure au kulipia.

Nini maoni yako msomaji wetu wa Teknokona kwa ujio wa Game hilo la Zlatan Ibrahimovic? Usisite kutuambia kitu hapo chini kwenye boksi la maoni.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.