Kia mwaka Apple inatoa toleo jipya la iPhone ambapo ndio kipindi ambacho huwa wanafanya uzinduzi mkubwa wa bidhaa zao na mara nyingi shughuli hiyo hufanyka mwezi Septemba kila mwaka.
Hivi sasa iPhone 13 ndio toleo la simu janja ambalo linaitambulisha vyema Apple lakini haiko peke yake bali zipo nyinginezo ambazo zilizinduliwa kwa pamoja mwezi Septemba 2021. Simu hiyo ambayo inamwagiwa sifa nyingi kwenye mitandao mbalimbali imepatikana na shida ya kifufundi kiasi cha kufanya walionazo kushindwa kuzitumia.
iPhone 13 imekumbwa na tatizo la kioo chake kubadilika rangi na kuwa Udhurungi huku kiini cha tatizo kikiwa hakijulikani. Watumiaji wa simu hiyo mmoja alibainisha kuwa tatizo lilianza wakati ambapo rununu husika ilishindwa kutoa mrejesho sahihi wa mahali alipokuwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa (GPS) kisha ikabadilika rsngi na kuwa Udhurungi (pink)! Mtu mwingine aliyekumbwa na tatizo hilohilo yeye alibainisha kuwa betri ya simu hiyo ilianza kufanya ndivyo sivyo kiasi kwamba rununu ikawa inagandaganda na mwishowe kubadilika rangi.

Je, tatizo hilo limesambaa kwa watu wengi duniani?
Tatizo la kioo kubadilika rangi limeonekana kuwakumbuka wateja waliopo Uchina na mara baada ya Apple kupata malalamiko ikabidi wawashauri wateja kupitia mtandao wa Weibo wahifadhi vitu vyao vya kwenye simu (backup) kisha wapakue toleo la karibuni kabisa la iOS na kuongeza kuwa tatizo hilo haliusiani na kifaa chochote ndani ya simu.
Katika masasisho yaliyotoka (iOS 15.3) toleo la majaribio haijaonekana Apple kuja na suluhu ya tatizo hilo. Kama tatizo hilo litaenea kwa watumiaji wengineo basi si vibaya ukahifadhi vitu vya kwenye iPhone 13 na kuhakikisha simu yako haidaiwi kushusha masasisho.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.