fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps instagram Teknolojia

Instagram kuwasaidia wenye Uraibu / ‘addiction’ wa utumiaji wa app hiyo

Instagram kuwasaidia wenye Uraibu / ‘addiction’ wa utumiaji wa app hiyo
Spread the love

Instagram kuwasaidia wenye uraibu (addiction) kwenye matumizi ya app hiyo maarufu. Kampuni ya Meta, mmiliki wa Facebook, Instagram na apps zingine maarufu, imesema inachukua hatua kupunguza utumiaji mbaya wa app hiyo.

Huduma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Take a Break’, itaanza kwenye mataifa ya Marekani, Uingereza, Ireland, Kanada, Australia, na New Zealand kabla ya kusambaa katika mataifa mengine yote. Huduma za Facebook na Instagram kwa kipindi kirefu zimekuwa zikilaumiwa kwa kusababisha na kulea matumizi mabovu, hasa hasa yanayohusisha vijana. Kupitia huduma hii Meta wanaonesha kujali afya za watumiaji wake hasa hasa vijana wadogo.

SOMA PIA  Samsung yaweka rekodi kwa kupata faida ya mamilioni ya dola ndani ya siku moja

Tayari ili kupunguza uraibu Instagram ilifanya mabadiliko katika masuala kuonesha ‘Likes’ za kwenye picha, baada ya kuonekana vijana wengi wakiangaika na kujaribu kufanya lolote ili waweze kupata Likes nyingi.

Instagram kuwasaidia wenye Uraibu

Instagram kuwasaidia wenye Uraibu

Kupitia huduma hii mpya watumiaji wataweza kuweka mpangilio (setting) ya kukumbushwa kupumzika kila baada ya dakika 10, 20 au 30 za utumiaji wa app ya Instagram.

SOMA PIA  Jamaa Avunja Vunja iPhone Na Mac Katika Apple Store Huko Ufaransa!

Tuendelee kutegemea kuona mabadiliko mengi kwenye huduma za Facebook na Instagram, kampuni mama ya Meta inapitia changamoto kadhaa na vyombo vya kisheria kuhusu jinsi huduma hizi za kijamii zinavyoathiri vijana.

Vyanzo: Meta, CNN

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania