Watu wengi wamekuwa wakihangaika namna ya kuhamisha namba za simu kutoka simu ya Android kwenda simu ya iPhone au kutoka simu ya iPhone kwenda simu ya Android, licha ya hivyo kuna njia kadhaa za kurahisha zoezi hilo na kukwepa upotevu wa namba za simu pindi unapoamua kubadili simu kutoka Android kwenda iPhone.
Ili kuhamisha namba za simu kutoka simu ya Android kwenda simu iPhone unaweza kusanikisha (install) programu maalumu ya Apple iitwayo “Move to iOS” iliyopo kwenye Google Play Store ya Android. Unaweza pia ukahamisha faili (file) la namba ya simu kwa njia ya VCF kutoka simu ya Android kwenda simu ya iPhone.
1. Kuhamisha namba za simu kutoka Android kwenda iPhone kwa njia ya “Move to iOS“
Apple wana programu (Application) inayoitwa “Move to iOS” inayopatikana kwenye Google Play Store ya simu ya Android, hii ni nzuri sana lakini hufanya kazi tu wakati wa kuanzisha iPhone mpya (setting up a new iPhone), huwezi kutumia Programu hii ikiwa tayari umeshapita kwenye hatua za awali za kuanzisha iPhone yako.
Kwanza pakua/download programu ya “Move to iOS” kwenye simu yako ya Android, wakati wa kuifungua hiyo programu itakuomba uipe ruhusa ya kutumia sehemu (permission to access your location) pamoja na kutuma jumbe (notifications) kwenye simu yako.
Baada ya hapo nenda kwenye simu ya iPhone kwenye sehemu ya mipangilio/settings kisha chagua sehemu ya “Move Data from Android” ukifungua hapo utapewa tarakimu sita (six-digit code) za kuingiza kwenye programu ya “Move to iOS” kwenye simu yako ya Android.
Baada ya kuingiza hizo namba sita utaona orodha ya vitu mbalimbali vya kuhamisha, hakikisha umechagua “Contacts” kisha bofya “Continue”.
Ikimaliza uhamisha utabofya sehemu ya “Done” ili kukamilisha zoezi hilo.
2. Kutumia njia ya “Google Sync” kupata namba za simu kutoka Android kwenda iPhone.
Ikiwa namba zako za simu zilikuwa zinatunzwa kwenye Google akaunti basi huhitaji tena kuhamisha unahitaji kuweka akaunti yako ya Google kwenye simu ya iPhone kisha unaruhusu (Sync) namba za simu kuonekana kwenye simu yako ya iPhone.
Kwanza fungua sehemu ya Settings kwenye simu ya iPhone.
Shuka chini mpaka sehemu ya “Contacts”
Chagua “Accounts.”
Kama hauna akaunti ya Google bofya “Add Account.” ili uweke akaunti, ila kama unayo bofya kwenye akaunti yako na uendelee mbele.
Ukubofya kwenye “Add Account” utachagua Google kwenye orodha ya huduma zilizopo, fuata maelekezo mpaka umalize kuweka akaunti ya Google.
Baada ya kuweka akaunti ya Google utaletewa machagua machache ya kuruhusu, hakikisha umeruhusu “Contacts”
Baada ya hapo utaona namba zako zote zinakuja kwenye simu ya iPhone.
3. Kuhamisha namba za simu kutoka Android kwenda iPhone kwa kutumia Faili (File).
Hii ni moja ya njia rahisi kabisa ambayo hutumiwa mara kwa mara, unaweza kutengeneza Faili la namba za simu kwenye simu ya Android kisha ukatuma kwenye simu ya iPhone na ukatapa namba kwa njia rahisi kabisa.
Nenda kwenye “Google contacts” kwenye simu yako ya Android, kama hauna unaweza kupakua (Download) programu ya “Google contacts” kwenye simu ya Android. ukifungua programu ya Google contacts nenda sehemu ya “Fix & Manage” kisha bofya “Export to File.”
Baada ya hapo utaona faili la Contacts.vcf chagua sehemu ya kutunza hilo faili kisha bofya kwenye SAVE
Ili kupata hilo faili kwenye simu yako ya iPhone unaitaji kutuma kutoka simu ya Android kwenda simu ya iPhone kwa njia ya Blutooth au email au njia nyingine.
ukishatuma faili kwenye simu ya iPhone, utafungua faili na hakikisha unafungua kwa kutumia programu ya “Contacts”
Baada ya hapo utafungua file na utaziongeza namba zako zote kwenye simu ya iPhone.
Kubadili simu kutoka Android kwenda iPhone siyo tatizo, tatizo kubwa linakuja unapotaka kuhamisha vitu kutoka simu yako ya zamani yaani Android kwenda simu mpya ya iPhone, hizo hapo juu ni njia za kuhamisha namba za simu kutoka Android kwenda iPhone.
kwa maoni zaidi unaweza kutuandikia kwenye sehemu ya comments
Unaweza pia kusoma makala zetu zingine hapa.
No Comment! Be the first one.