Mitandao ya kijamii ambayo inaongelewa hapa katika maswala ya tiki ya bluu ni Facebook na Instagram ambayo yote iko chini ya kampuni ya Meta.
Ni wazi kwamba mitandao mingi ya kijamii kwa sasa inapitia magumu, kumbuka huduma ya kulipia ili upate tiki ya blue hata katika mtandao wa twitter imefanyika hivyo hivi karibuni, Meta nao hawataki kubaki nyuma.
Huduma hii inakua ni ya kulipia kwa mwezi, na kingine kizuri ni kwamba mitandao hiyo kama kawaida itakua inapatika bure kama kawaida ili kama ikitokea ulikipia kuna vitu vitaongezeka.
Hii ni kama huduma ya Twitter Blue kutoka Twitter maana huduma ya Twitter inapatikana bure lakini kunakua na kitu ambacho kinaongezeka katika swala zima la huduma.
Meta Verified Itakua Na Huduma Hizi
- Utapata tiki ya Bluu kuonyesha kama uko ‘verified’.
- Uzuizi wa kufungua akaunti yako kwa majina yako (kama ilivyo kwa wasanii na watu maarufu).
- Utapata msaada wa haraka kutoka kwa huduma kwa wateja.
- Utapata upendeleo katika eneo la comments (comments zako zitakua zinaonekana sana kuliko za wengine).
- Mambo yako yataonekana kwa urahisi katika eneo la Explore na Reels.
- Utapata Stickers maalum kwenye IG Stories ambazo ambao hawajalipa hawatazipata.
Kingine ni kwamba sio wote ambao wanaweza kupata huduma hii, ili kupata huduma hii ni lazima vigezo vifuatavyo vizingatiwe.
- Hairuhusiwi kwa page za biashara
- Lazima uwe na zaidi ya miaka 18
- Lazima uwe na Profile picture ambayo inaonyesha picha yako
- Page iwe active – inatumika mara kwa mara
- Uwe na uthibitisho wa kitambulisho cha serikali
Kingine cha kushangaza ni kwamba gharama za malipo kwa upande wa mtandao (kwa kupitia kompyuta) ni tofauti kabisa na zile za kupitia katika App zake za simu.
Meta Verified itakua na utofauti wa gharama maana katika Android na Apple kutakua na gharama ya ziada ambayo inaenda kwa kampuni zenye masoko hayo ili kutofautisha na kujiunga kupitia katika mtandao.
huduma hii haijaanza kupatika katika maeneo mengi, kwa kuanzia tuu yametengwa maeneo machache kwa kuanzia kupatikana kwa huduma hii na kisha baadae itasambaa zaidi
Chanzo: @itsApollo/@Swahili.tek Na Mitandao Mingine
Je uko tayari kuanza kutumia huduma ya Meta Verified? Niandikie hapo chini katika eneo la comment? je unadhani pia kampuni itapata mapato mengi zaidi kwa kupitia huduma hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.