Hatimaye Apple wameamua kuwaondolea tatizo la chaji watumiaji wake baada ya kuwapa uwezo wa kupunguza matumizi ya betri katika simu. Toleo jipya la mfumo endeshaji wa simu wa iOS 9 linalotegemea kutoka mwezi wa tisa pamoja na mambo mengine litakuwa na uwezo wa kupanga matumizi ya betri yako ya simu au tableti kwa kiwango kikubwa.
Chaji ni homa ya kila mmiliki wa simu janja, tunalazimika kubeba chaja zetu ama betri za akiba mara kwa mara. Kwa watumiaji wa iPhone pia hali ni mbaya, yaani huwezi kushinda kutwa na ukiwa umewasha data katika simu bila kuchaji, ni lazima betri yako itaisha halikadharika kwa watu ambao muda mwingi wanakuwa katika maongezi katika simu hizo.
Toleo jipya la iOS 9 lililo katika hatua ya majaribio hivi sasa litaleta uwezo kwa watumiaji wa simu kuweza kuzipangia simu zao matumizi ya betri na hivyo kuongeza muda wa kudumu chaji katika simu zao. Kinachotokea ni kwamba pindi tu mfumo huu unapowashwa basi kwanza utapunguza uwezo wa simu yaani mwendo kasi wake, pili utaathiri uwezo wa skrini (baadhi ya manjonjo yatapungua), tatu itazizuia programu zinazoendeshwa chini kwa chini, nne barua pepe hazitashushwa bila ruhusa yako na mwisho mipakuo inayojiendesha (automatic downloads ) pia itazuiliwa mpaka pale utapokuwa umeichaji simu yako.
Tunazidi kuona mambo mengi mazuri yakizidi kufanyika katika kuhakikisha simu zetu zinakaa na chaji muda mrefu zaidi.
Soma Pia – Samsung Kuleta Simu Zenye Betri ya Kukaa na Chaji Muda Mrefu Zaidi
Kwa maoni maswali na ushauri usisite kutufuata katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii :- Instagram | Twitter | Facebook
No Comment! Be the first one.