Simu za Huawei kutumia zaidi Kirin badala ya Qualcomm

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Simu nyingi za Huawei ambazo zipo tayari sokoni zinazotumia Kirin (kipuri mama) ni chache ukilinganisha na zile ambazo zinatumia aina nyingine ya vipuri lakini hilo linatazamiwa kubadilika katika nusu ya pili kwa mwaka 2019.

Huawei wamekuwa wakinunua vipuri mama kutoka kwa makampuni mbalimbali na kutumia kwenye simu janja wanazotoa kulinganisha na zile ambazo zimewekwa Kirin ikiwa kama ndio “Ubongo” wa simu husika. Mambo yanatarajiwa kuwa tofauti kidogo hasa kwa simu janja ambazo zitatoka kwenye robo ya pili  mwaka huu; kwa lugha rahisi zitatumia Kirin zaidi badala ya Qualcomm.

badala ya Qualcomm

Kipuri mama cha Kirin kutumika zaidi kwenye simu za Huawei badala ya Qualcomm ambazo zitatoka kwenye robo ya pili mwaka huu.

Takwimu zinaonesha kuwa nusu ya pili mwaka 2018 Huawei walitumia pungufu ya 40% kwa vipuri vya Kirin SoCs wanavyotengeneza wao wenyewe huku nusu ya kwanza mwaka 2019 walitumia kipuri cha Kirin kwa 45%. Sasa kwa robo ya pili zaidi ya milioni 150 za simu za Huawei zitatumia kipuri cha Kirin huku ikiwa na mpango wa kuuza maeneo mbalimbali simu janja 270 milioni mwaka huu ambapo hiyo yote ni sawa na 60%.

INAYOHUSIANA  Upatikanaji wa Infinix Zero 6 warahisishwa nchini Tanzania

Huawei wameamua kuweka nguvu kubwa zaidi kwenye kipuri wanachotengeneza weyewe kwa sababu ya kutaka kupunguza utegemezi kutoka kwa makampuni mengine mathalani wanaotengeneza MediaTek na Qualcomm.

badala ya Qualcomm

Moja ya simu janja zinazotumia Kipuri mama-Kirin.

Ndio hivyo Huawei wameamua kutumia vya kwao zaidi na hivi karibuni wametoa Kirin 810 sasa basi tutegemee kuona simu janja nyingi zikitumia vipuli vya kwao zaidi.

Vyanzo: GSMArena, Tech Lapse

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.