fbpx

Bluetooth 5: Uwezo wa utumaji mafaili mbali zaidi, kwa kasi zaidi unakuja

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Moja ya teknolojia muhimu katika vifaa vya mawasiliano vya kielektroniki kwa watumiaji wengi ni teknolojia ya Bluetooth.

Teknolojia ya bluetooth ni moja ya teknolojia muhimu katika harakati za sasa za utengenezaji zaidi wa teknolojia zinazorahisisha mawasiliano ya kati ya kifaa kimoja hadi kingine cha elektroniki – IoT (Internet of Things).

bluetooth 5

Kutuma mafaili kati ya simu kwa simu – kompyuta kwa kompyuta – simu kwa kompyuta – kompyuta kwa simu – utumiaji wa earphones/headphones za bila waya na matumizi mengine mengi..teknolojia ya bluetooth ni muhimu sana.

Bodi inayosimamia muendelezo wa teknolojia ya Bluetooth (Bluetooth SIG – Bluetooth Special Interest Group) imepitisha rasmi teknolojia ya kisasa zaidi ya bluetooth – Bluetooth 5, na tegemea vifaa mbalimbali hasa hasa simu mpya za ndani ya miezi 3 -4 ijayo kuanza kuja nayo.

bluetooth

Toleo la Bluetooth 5 linamaboresho yafuatayo;

  • Kufika umbali zaidi ya mara nne ukilinganisha na mwisho wa signal za bluetooth kwa sasa
  • Kasi ya utumaji mafaili wa mara mbili zaidi ukilinganisha na sasa
  • Kingine pia ni pamoja na upunguzwaji wa muhingiliano wa mawimbi ya mawasiliano dhidi ya teknolojia zingine za mawasiliano.

*Kwa sasa tolea la kisasa la teknolojia ya bluetooth ni Bluetooth 4.2

Bodi hiyo pia imerahisisha utambuaji wa teknolojia ya Bluetooth iliyokwenye kifaa kabla ya mtumiaji kununua. Kwa mfano kwa sasa teknolojia ya Bluetooth 4 inafahamika kwa majina mengi sana; Bluetooth LE, BLE, Bluetooth Smart na mengine mengi. Bluetooth 5 itafahamika kama Bluetooth 5 tuu, hakuna mwenye ruhusa ya kuipa jina jingine.

Wengi wanategemea katika makampuni yatakayowahi kuja na teknolojia hizi basi Apple na Sumsang hawawezi kukosekana, hasa hasa Apple.

Je wewe unatumiaje teknolojia ya bluetooth iliyokwenye simu yako? Je unafikiri bado ni muhimu kwa matumizi yako ya kila siku?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Go Green; App mahususi kwa ajili kukupa dondoo jinsi ya kutunza vitu mbalimbali
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.