IFA 2017. Onesho kubwa la uuzaji, na utambulisho wa vifaa ya kielektroniksi la bara la Ulaya Maarufu kama IFA (Internationale Funkausstellung Berlin) linatarajiwa kuzinduliwa Septemba mosi mwaka huu.
IFA 2017 inafanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani, makampuni makubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani yatashiriki ili kuonesha bidhaa zao wanazotaraji kuzitoa siku za karibuni.
Kuanzia Simu Janja, Laptops, TV, Radio, Mashine za kufulia nguo, majiko ya umeme, Mafriji na vifaa vingine vingi vinataraji kuuzwa na kutangazwa.

IFA ni moja ya maonesho ya kale zaidi ya viwanda tangu mwaka 1924 likiwa linafanyika kila mwaka, hususani mwezi Septemba. Kwa sasa onesho hilo limekuwa maarufu kwa vifaa vya umeme na majumbani pia.
IFA inatoa fursa kwa makampuni kuwasilisha bidhaa zao na maendeleo ya uzinduzi wa bidhaa mpya. Kwa mara ya kwanza IFA ya mwaka huu inatarajiwa kuwa sehemu ya uzinduzi wa bidhaa nyingi kuliko miaka iliyopita.
One Comment
Comments are closed.