fbpx

apps, Mtandao wa Kijamii, Video, YouTube

YouTube yafanya mabadiliko ya logo!

youtube-yafanya-mabadiiko-ya-logo

Sambaza

YouTube yafanya mabadiiko ya logo. Huu ni muendelezo wa maboresho mbalimbali ambayo YouTube imekuwa ikiyafanya ili kuboresha huduma zake kwa watumiaji wake wa kompyuta na simu janja. 

Mabadiliko hayo yana siku chache ambapo yanahusisha logo na mpangilio wa video na muonekano wa matangazo.

Mabadiliko ya logo ya YouTube yashafanyika mara kadhaa lakini kwa sasa ndio yatakuwa mabadiliko makubwa. Muonekano wa logo wa sasa kumewekwa alama ya batani ya kucheza (Play).

INAYOHUSIANA  Namna ya kurudisha picha/video ulizovifuta kwenye simu za Android/iOS #Maujanja
Orodha ya mabadiliko ya logo za YouTube kwa miaka kadhaa.

YouTube yafanya mabadiiko ya logo.

Muonekano wa Logo yake ya zamani ni ule wa neno lake la ‘Tube’ kuwa ndani ya kiboksi kilichokuwa kinawakilisha muonekano wa TV, kwa sasa kiboksi hicho kitajitegemea na kitakuwa nje ya neno ‘YouTube’.

Mabadiliko haya ya YouTube yamezingatia kuifanya kuwa na wepesi zaidi pale mtu anapofungua kurasa za YouTube. Hasa hasa kwa watumiaji wa simu za mkononi.

INAYOHUSIANA  Soko la apps za Android, Google Playstore kupatikana kwa watumiaji wa Chrome OS
youtube
Tayari maboresho yamefanyika kwenye muonekano wa tovuti ya YouTube
YouTube yafanya mabadiiko ya logo
YouTube yafanya mabadiliko ya logo : Muonekano wa logo mpya

Mabadiliko hayo tayari yapo kwenye kompyuta na Simu yakiendelea kadri yalivyopangwa. Mabadiliko hayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na watumiaji wa YouTube. Wapo waliofurahi mabadiliko hayo na kusema yapo safi.

Lakini wapo walioponda na kusema ni bora ungebaki muonekano ule wa awali kwani ulikuwa mzuri zaidi kuliko wa sasa.

Pia wapo waliosema ni bora wangebadili tu muonekano wa Logo na muoenekano wa ukurasa ungebaki kama awali.

Je msomaji wetu umeyaona mabadiliko hayo ya YouTube? Kama umeyaona nini maoni yako. Je mazuri au wamechemsha.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.