Ni kawaida kabisa namba zetu za simu kujihifadhi katika akaunti zetu za goole na icloud. Mara kwa mara shida inakuja pale unapotaka kubadilisha kifaa na kwenda katika mfumo mwingine (iOS-Android).
Kuhamisha namba hizi za simu kutoka sehemu moja kwenda nyingine kunahusisha hatua mbili ambapo unaweza kuchagua mwenyewe.
Unaweza hamisha taarifa za mawasiliano kutoka au kwenda Gmail (google) au kwenda au kutoka iOS (iPhone). Na hazi hapa chini ndio njia za kufuata.
Kutoka iCloud (iOS/iPhone)
Ingia katika mtandao wa iCloud.Com kwa kutumia kompyuta na kisha nenda katika eneo la ‘contacts’ na kishafungua.

Ukishafungua shikilia Ctrl+AÂ kwa sekunde kadhaa ili kuchagua majina (na mawasiliano yake) na kisha ingia katika kialama cha ‘setting’ upande wa chini kushoto kabisa. Baada ya hapo chagua ‘Export vCard’ ili kuanza kuhamisha taarifa hizo.

Kwenda Android (Gmail/Google)
Mpaka hapo unakua tayari una faili la namba za simu katika kompyuta yako (litakua limeshajishusha katika kompyuta) na hapo ndio hatua za kulipandisha katika gmail (google) inabidi zianze.

Sasa Basi ingia katika akaunti yako ya Gmail na kisha fika eneo la ‘contacts’ au unaweza ingia moja kwa moja kupitia Accounts.google.com
Nenda katika ‘menu’ ambayo iko upande wa kushoto na kisha chagua ‘import’ ili kuanza kufanya zoezi hilo.

Chagua faili la namba (mawasiliano) ambalo lilishuka katika kompyuta yako na kisha anza kulipandisha.

Mpaka hapo utakua umeshaweza kukamilisha hili, lakini pia kumbuka huduma hii inaweza ikabadilika kwani unaweza amua kuanzia unapotaka wewe (Android kwenda iOS anu iOS kwenda Android).
No Comment! Be the first one.