fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android 11 apps Samsung Teknolojia

Android 11 yagonga hodi kwenye simu janja Samsung Galaxy A30s

Android 11 yagonga hodi kwenye simu janja Samsung Galaxy A30s

Spread the love

Miaka miwili baadae tangu Samsung Galaxy A30s itoke sasa Android 11 imegonga hodi kwenye rununu husika ikikiwa ni muendelezo wa simu janja mbalimbali kuwa na uwezo wa kutoka kwenye toleo moja hadi jingine.

Mwaka 2019, Samsung Galaxy A30s ikiwa na Android 9 ambapo kwa wakati ule ndio ilikuwa habari ya wengi kwenye simu janja zinazotumia rogramu tumishi husika. Mwaka hadi mwaka toleo la Android likawa linatokka na sasa tupo kwenye Android 11.

SOMA PIA  Whatsapp Yapata Muonekano Mpya wa 'Material Design'

Kwa watumiaji wa Galaxy A30s hii ni habari njema kwao kwani sasa wanaweza kupakua Android 11 baada ya kuwa wavumilivu wakisubiri toleo hilo la programu endeshi husika pamoja na ile sura ya mbele (UI 3.1).

simu janja Samsung

Android 11 yafika kwenye Galaxy A30s: Toleo hilo linatambulishwa kwa mchanganyiko huu wa tarakimu A307FNXXU2CUF2.

Angalizo/Muhimu kufahamu

Suala la kupakua programu endeshi si kitu kigumu kabisa iwapo utazingatia mambo muhimu kabla ya kuanza zoezi zima. Kwanza kabisa ni lazima kuhakikisha simu janja ina chaji kuazia 50% na kuendelea, ina nafasi/memori angalau GB 1.5 au zaidi. Kitu cha muhimu na pengine uti wa mgongo wa kufanikisha suala zima hakikisha una kifurushi cha intaneti angalau GB 1.3 na kuendelea.

SOMA PIA  PlayStore Kutoonyesha Masasisho (Updates) Ya #App Tena Ktk Notification!

Leo imekuwa ni zamu ya rununu hii je, kesho itakuwa ni simu gani? Jibu ya hilo swali ni kuendelea kutufuatilia kila siku ili kuweza kuhabarika.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania