Toleo lijalo la Windows linategemewa kutolewa Jumanne hii, tarehe 30 mwezi huu. Jina kamili la Windows 9 limetajwa rasmi na rais wa Microsoft Ufaransa Bwana Alain Crozier, alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kuhusu tukio la tarehe 30 mwezi wa tisa.
“Muda kama huu mwaka jana tulitambulisha Windows 8…siku chache zijazo tutatambulisha Windows 9”, alisema Bwana Alain.
Kitu kikubwa kinachoonekana kwa sasa ni mabadiliko ambayo kampuni ya Microsoft inapitia chini ya uongozi wa Satya Nadella kutoka CEO wa zamani Bwana Steve Ballmer. Chini ya Steve Ballmer Microsoft ilizidisha nguvu katika Windows na utengenezaji wa vifaa (kompyuta, simu na tableti), lakini kwa sasa uongozi wa Satya Nadella Microsoft inaongeza nguvu pia katika kuboresha utoaji wa huduma zake kama programu ya Office kwenye vifaa vingine kama tableti na simu-janja.
Je Mabadiliko Gani Yanakuja?

Windows 8 ilitengenezwa kwa kufikiria tableti na vifaa vya mshiko (Touch) na kutokana na hili kulikuwa na malalamiko mengi kutoka kwa watumiaji wa kompyuta za kawaida na zile za mpakato. Moja ya mabadiliko makubwa yanayotegemewa kuja kwenye Windows 9 ni kurudishwa kwa muonekano wa ‘Start’ kuwa kama zamani enzi za Windows 7, Vista na XP.
Mabadiliko mengine bado hayajajulikana kwa sasa.
Windows 8 Bado Haifanyi Vizuri
Katika asilimia ya utumiaji bado Windows 7 inaongoza kwa kutumika kwa takribani zaidi ya asilimia 50 wakati Windows 8 ipo katika asilimia 12% na Windows XP ikiwa na asilimia 25%. Inasemekana kwa mwaka 2013 takribani asilimia 68 ya kompyuta ziliuzwa zikiwa na Windows hii ikiwa ni chini zaidi kutoka asilimia 75.2 kwa mwaka 2012.
Ingawa soko la kompyuta asa za mpakato lilikuwa mwaka huu inasemekana ukuaji wote ulitokana na uuzaji wa kompyuta za Macs na Chromebooks. Uuzaji wa Chromebooks ulipanda kutoka asilimia 0.2Â kwa mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 4 katika kompyuta zote zilizouzwa kipindi cha mwaka 2013. (~Takwimu kutoka Net Applications na NPD Research Group)
Je Windows 9 inaweza kuleta mafanikio kwa Microsoft? Jibu tutalipata siku chache zijazo.
{MPYA SOMA – MICROSOFT WARUKA WINDOWS 9 NA KUJA NA WINDOWS 10}
No Comment! Be the first one.