fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu

Hizi Ndizo Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa!

Hizi Ndizo Simu 20 Zilizouzika Zaidi Duniani Hadi Sasa!

Spread the love

Je unafikiri ni iPhone au Samsung ndio wametengeneza simu zilizouzika zaidi? Soma hapa kuzitambua simu 20 zilizouzika zaidi katika historia.

Tutaanza na ya 20 kwenda hadi ya kwanza,

Nokia3100

Nokia 3100 Inashika Nafasi ya 20

 

Namba 20: Nokia 3100 (3120)

Ilitolewa Mwaka: 2003

Idadi ya Mauzo: Milioni 50

Nafasi ya 19 inashikiliwa na iPhone 5S kutoka Apple.

iPhone 5S iliyoingia Sokoni Mwaka 2013 yashika Nafasi ya 19

iPhone 5S iliyoingia Sokoni Mwaka 2013 yashika Nafasi ya 19

Namba 19: iPhone 5S

Ilitolewa Mwaka: 2013

Idadi ya Mauzo: Milioni 52

Nafasi ya 18 inashikiliwa na Samsung kupitia Samsung Galaxy S III

Samsung Galaxy SIII iliingia Sokoni kati kati ya mwaka 2012

Samsung Galaxy SIII iliingia Sokoni kati kati ya mwaka 2012

Namba 18: Samsung Galaxy SIII

Ilitolewa Mwaka: 2012

Idadi ya Mauzo: Milioni 60

Namba 17 inarudi kwa Apple kupitia iPhone 4S iliyoingia sokoni Oktoba mwaka 2011, ilifanikiwa kuvunja rekodi ya kimauzo ya haraka kwa iphones kutokana na kufanikiwa kuuza zaidi ya milioni 5 ndani ya siku 5, milioni moja ikiwa ni malipo ya ndani ya masaa 24 kabla ya simu kuingia sokoni rasmi (pre-order). Pia mwanzilishi mashuhuri wa kampuni ya Apple, Steve Jobs, alifariki siku moja baada ya ujio wa iPhone 4S kutangazwa rasmi.

Muonekano wa iPhone 4s Nyeusi

Muonekano wa iPhone 4s Nyeusi

Namba 17: iPhone 4s

SOMA PIA  Mambo ya kuzingatia unapotaka kupakua App Playstore

Ilitolewa Mwaka: 2011

Idadi ya Mauzo: Milioni 60

Namba 16 inashikiliwa na StarTAC kutoka Motorola! Muhimu hapa ni kwamba StarTac iliyotoka mwaka 1996 ndiyo simu ya kwanza kununuliwa kwa wingi duniani. Na kwa kuingia sokoni mwaka 1996 inakuwa ndiyo simu ya zamani zaidi katika orodha hii, na hii ndiyo simu ya kwanza kabisa kuwa ya kufunga (Flip).

Motorola ndiyo ilikuwa kampuni ya kwanza kutengeneza simu ya mkononi iliyouzika kwa wingi zaidi: StarTAC

Motorola ndiyo ilikuwa kampuni ya kwanza kutengeneza simu ya mkononi iliyouzika kwa wingi zaidi: StarTAC

Namba 16: StarTAC

SOMA PIA  Miaka 10 ya iPhone: Simu bilioni 1.2 zimeshauzwa

Ilitolewa Mwaka: 1996

Idadi ya Mauzo: Milioni 60

 

Namba 15 inashikiliwa na simu kutoka Motorola tena, nayo ni Motorola C200. Haikuwa na mvuto sana, ila iliuzika! Nakumbuka kuziona simu hizi miaka ileeee.

Tanzania_Motorola_c200

Motorola c200

Namba 15: Motorola C200

Ilitolewa Mwaka: 2006

Idadi ya Mauzo: Milioni 60

 

Nokia 5130 (5220/5310) inashika nafasi ya 14, na naamini ata wewe utakuwa unakumbukumbu nayo hii. Kama si wewe mwenyewe kutumia basi uliiona kwa sana. Ilipata umaarufu zaidi kutokana na uzuri wake na uwezo wake mzuri kwenye utumiaji wa intaneti na kusikilizia muziki. Ikiwa na sifa zile zile Nokia walitofautisha maumbo kwa matoleo ya 5220 na 5310.

Muonekano wa Nokia 5130 xpressmusic

Muonekano wa Nokia 5130 xpressmusic

Namba 14: Nokia 5130

Ilitolewa Mwaka: 2007

Idadi ya Mauzo: Milioni 65

SOMA PIA  Ifahamu 'Menu' Ya Siri Ya Majaribio Katika Simu Za Samsung Galaxy!

Nafasi ya 13 inabebwa na Nokia tena, na hii ni kupitia Nokia 6010 (6020/6030) iliyotoka mwaka  2004, na hii ni moja ya simu ambayo hata kwetu ilitumika sana enzi zile.

Nokia 6010 iliyotoka mwaka 2004

Nokia 6010 iliyotoka mwaka 2004

Namba 13: Nokia 6010

Ilitolewa Mwaka: 2004

Idadi ya Mauzo: Milioni 75

 

Nafasi ya 12 inashikiliwa na iPhone 5 kutoka Apple, hii iliingia sokoni mwaka 2012. iPhone 5 ilikaribisha mabadiliko makubwa kufananisha na matoleo ya nyuma ya iPhone kama iPhone 4 na zinginezo, hii ilikuwa ni pamoja na kupata kioo kikubwa zaidi na pia mabadiliko ya utumiaji wa waya wa kuchajia.

Muonekano wa iPhone 5 Nyeusi

Namba 12: iPhone 5

Ilitolewa Mwaka: 2012

Idadi ya Mauzo: Milioni 91*

Namba 11 inashikiliwa na Nokia 1208 (1209) iliyoingia sokoni mwaka 2007. Hii ni maarufu kweli, mwenyewe nishawahi itumia na nina uhakika vijana wa miaka ya 2008-10 wote watakuwa wameitumia au kuiona. Ingawa haikuwa na sifa za kisasa zaidi wengi waliipenda kutokana na uwezo wa kukaa na chaji muda mrefu na pia uwepo wa tochi ya bure.

Muonekano wa Nokia 1208, ulishawahi kuitumia?

Muonekano wa Nokia 1208, ulishawahi kuitumia?

Namba 11: Nokia 1208

Ilitolewa Mwaka: 2007

Idadi ya Mauzo: Milioni 100

Je ushawahi kutumia simu ipi kati ya hizi tulizozipitia?

(BOFYA KUSOMA NAMBA KUMI HADI 1 KWA KUBOFYA HAPA)

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania